logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ubalozi wa Marekani watoa ilani kwa raia wake kutosafiri Kisumu wakati wa uchaguzi

Ilidaiwa kwamba maandamano na mikutano ya hadhara inayohusiana na uchaguzi hufanyika mara kwa mara kitu ambacho rai wa Marekani wanahofia.

image
na Radio Jambo

Habari03 August 2022 - 06:58

Muhtasari


•Maandamano haya yanaweza kuwa ya vurugu, na kulazimisha polisi kuingilia kati.

Lango kuu ya Ubalozi wa Marekani

Ubalozi wa Marekani mjini Nairobi umewaonya raia wa Marekani dhidi ya kusafiri hadi Kisumu wakati wa uchaguzi.

Kenya imeratibiwa kufanya uchaguzi mnamo Agosti 9, 2022 huku kampeni za afisi za mashinani na kitaifa zikiendelea kikamilifu.

Kenya imekuwa ikikumbwa na ghasia za kabla ya uchaguzi mara kwa mara wakati wa mizunguko ya uchaguzi.

Ilidaiwa kwamba maandamano na mikutano ya hadhara inayohusiana na uchaguzi hufanyika mara kwa mara kitu ambacho rai wa Marekani wanahofia.

Maandamano haya yanaweza kuwa ya vurugu, na kulazimisha polisi kuingilia kati.

Baadhi ya matokeo mabaya ya migomo na shughuli nyingine za maandamano uchangia  hali duni  ya kiuchumi nchini.

Wizara ya mambo ya nje inawakumbusha raia wa Marekani kuhusu usalama wao na kuendelea kuwa macho kuhusu shughuli zote za uchaguzi.

Kwa sasa Balozi wa Marekani nchini Kenya ni  Meg Whitman ambaye alithibitishwa katika kura ya kauli moja na Seneti ya Marekani kama balozi wa kumi na nane wa Marekani nchini Kenya mnamo Julai 14, 2022.

Whitman pia amekuwa mwanachama wa idadi ya bodi za wakurugenzi za mashirika, ikiwa ni pamoja na Procter & Gamble na General Motors.

Juhudi zake umeonekana kwa kujitolea kupigania usawa katika elimu na ulinzi wa mazingira, Balozi Whitman amekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kitaifa ya Kufundisha


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved