In Summary

•Wanafunzi hao walikanusha mashtaka walipofika mbele ya Hakimu Mkuu Onkoba Mogire Eldoret

•Anthony Fedha alikuwa ameitaka mahakama kuwapa washukiwa masharti makali ya bondi, ikizingatiwa uzito wa kosa hilo

Mahakama
Image: HISANI

Wanafunzi tisa wa Chuo Kikuu cha Moi wameachiliwa kwa dhamana ya KSh 500,000 pesa taslimu kila mmoja baada ya kukana kuchapisha habari za uongo na kuzua hofu.

Wote walikanusha mashtaka walipofika mbele ya Hakimu Mkuu Onkoba Mogire aliyeketi Eldoret. Kesi hiyo itatajwa Agosti 22.

Washukiwa hao ni pamoja na Ronald Odhiambo, Martin Rodgers, Josphat Chacha, Ian Muibanda, Brian Kipkorir, Denis Wakhanya, Beatrice Wanhari, Samwel Juma, na Ann Aoko.

Wakili wa Serikali Anthony Fedha ameitaka mahakama hiyo kutoa masharti magumu ya dhamana kwa watuhumiwa kwa kuzingatia uzito wa kosa hilo.

''Hatupingi masharti ya dhamana kwa washukiwa," alisema.

Wanafunzi hao tisa pia walikuwa wameiomba mahakama kuwapa masharti ya dhamana badala ya kuwafunga  kwa sababu ni wanafunzi kutoka kwa familia isiyoweza kifedha.

Wanafunzi hao walikamatwa kwa kusambaza ujumbe ya chuki kwenye vikundi vya WhatsApp.

Vijikaratasi vilivyozua taharuki vilionya baadhi ya jamii kuondoka kaunti ya Uasin Gishu kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9 iwapo hawatampigia kura mgombeaji fulani wa urais.

Mmoja wa wanafunzi hao aliambia mahakama kuwa wao hawakusambaza hizo vijikaratasi hizo kwa umma.

Kufuatia kukamatwa kwao mnamo Jumanne, Agosti 2, afisa wa uchunguzi Sophia Ibrahim aliomba mahakama kuwazuilia wanafunzi hao kwa ajili ya kufanya uchuguzi kuhusu matendo yao.

 

View Comments