In Summary
  • "Ingawa kwa kiasi kikubwa polisi wamejiendesha kwa mujibu wa sheria, Mamlaka imebaini matukio ya pekee yanayohitaji uchunguzi wake," alisema Bi Makori.
Anne Makori mwneyekiti wa IPOA

Mamlaka Huru ya Polisi na Usimamizi (IPOA) sasa imeanzisha uchunguzi kuhusu mienendo ya maafisa waliotumwa katika maeneo mbalimbali ili kuwezesha utendakazi mzuri wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Kulingana na IPOA, katika taarifa kwa vyumba vya habari iliyotiwa saini na Mwenyekiti Anne Makori siku ya Jumamosi, maafisa 250 wa polisi walitumwa wakati wa uchaguzi.

Licha ya kubainisha kuwa mwenendo wa jumla wa maafisa wengi umekuwa wa kupigiwa mfano, mamlaka hiyo hata hivyo ilitaja matukio matatu ambayo inasema tangu wakati huo imeanza kuchunguza.

Hizi ni pamoja na madai ya kupigwa risasi wanaume wawili na mwanamke mmoja na polisi huko Eldas, Kaunti ya Wajir; wahasiriwa walipata majeraha.

IPOA pia iliripoti tukio ambapo afisa mmoja katika Kituo cha Polisi cha Matisi katika Kaunti ya Bungoma alijaribu kumbaka raia mnamo Agosti 10, 2022.

Makori alisema kwamba inachunguza tukio la tatu ambapo afisa wa polisi katika Kaunti ya Uasin Gishu anadaiwa kumpiga risasi na kumjeruhi mlinzi wa mwaniaji wa kisiasa mnamo Agosti 8, 2022.

"Ingawa kwa kiasi kikubwa polisi wamejiendesha kwa mujibu wa sheria, Mamlaka imebaini matukio ya pekee yanayohitaji uchunguzi wake," alisema Bi Makori.

“IPOA pia inaangalia jinsi polisi wanavyoendelea kudhibiti umati, kudumisha usalama na utulivu katika kipindi hiki cha kuandaa uchaguzi. IPOA inasalia kujitolea kuwa huru, bila upendeleo na haki."

 

 

 

 

 

View Comments