In Summary

•Alisema familia itatoa taarifa ya kina na kushiriki mipango ya mazishi baadaye.

•Bw Koskei alitetea kiti chake kama mgombea  huru baada ya kushindwa katika kura za mchujo za UDA mnamo Aprili 14 na Bw Sigei.

Aliyekuwa mbunge wa Sotik Anthony Kimetto akiwahutubia wanahabari mjini Nakuru Oktoba 31, 2012.
Image: HANDOUT

Aliyekuwa mbunge wa Sotik Anthony Kipkosgei Kimetto amefariki.

Mbunge huyo wa zamani  alifariki katika Hospitali ya Nairobi, ambako alikuwa akipokea matibabu kwasababu ya matatizo ya kisukari.

Mwanawe, Mbunge wa Sotik anayeondoka Dominick Koskei, alithibitisha kufariki kwa babake.

"Ni kweli, Mzee ametuacha. Aliaga dunia Jumatatu alipokuwa akipokea matibabu," alisema Bw Koskei.

Alisema familia itatoa taarifa ya kina na kushiriki mipango ya mazishi baadaye.

Bw Kimetto, ambaye alihudumu kwa mihula mitatu kama mbunge wa Sotik katika Kaunti ya Bomet, alishindwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2007 na aliyekuwa waziri wa Mambo ya Ndani Lornah Chepkemoi Laboso.

Mwanawe Dominick Koskei alichukua uongozi kutoka kwa Bi Laboso  kama mbunge wa Sotik 2017 lakini akashindwa na aliyekuwa kamishna wa jimbo la Nairobi Francis Sigei wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) katika uchaguzi wa mwaka huu.

Bw Koskei alitetea kiti chake kama mgombea  huru baada ya kushindwa katika kura za mchujo za UDA mnamo Aprili 14 na Bw Sigei.

Kiongozi wa Chama Cha Mashinani (CCM) Isaac Ruto, aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki John Koech, Mbunge mteule wa Sotik Francis Sigei, mwenzake wa Bomet Mashariki Richard Yegon na Mwakilishi wa Wanawake wa Bomet anayeondoka Joyce Korir ni miongoni mwa waliotuma risala zao za rambirambi kwa familia hiyo.

 

View Comments