In Summary

•Kiraitu ambaye ni mwenyekiti wa Devolution Empowerment Party (DEP) aliwaongoza viongozi wengine wa chama hicho kwa mkutano na Muungano wa Kenya Kwanza.

•Kiraitu alipoteza azma yake ya kuwania ugavana wa Meru kwa muhula wa pili katika uchaguzi wa mwezi uliopita ambapo alishindwa na mgombea huru Kawira Mwangaza.

Devolution Empowerment Party (DEP) kikiongozwa na mwenyekiti Kiraitu Murungi wakikutana na wanachama wa Kenya Kwanza katika makazi ya DP William Ruto huko Karen mnamo Septemba 2, 2022.
Image: DPPS

Ijumaa aliyekuwa gavana wa Meru Kiraitu Murungi alitembelea rais mteule William Ruto katika makazi yake ya Karen, Nairobi.

Kiraitu ambaye ni mwenyekiti wa Devolution Empowerment Party (DEP) aliwaongoza viongozi wengine wa chama hicho kwa mkutano na Muungano wa Kenya Kwanza.

Ruto alisema kuwa chama cha DEP kimeamua kufanya kazi na muungano wake lakini gavana huyo wa zamani bado hajazungumzia suala hilo.

"Tunakaribisha Devolution Empowerment Party (DEP) katrika Kenya Kwanza. Kufanya kazi nasi ni azimio ambalo a viongozi wanakubali,” Ruto alisema.

Viongozi waliohudhuria ni pamoja na Naibu Rais Mteule Rigathi Gachagua, Musalia Mudavadi, Moses Wetang'ula, Salim Mvurya, Aden Duale, Cecily Mbarire, Justin Muturi, Lenny Kivuti, Kathuri Murungi, Moses Kirima, Mugambi Rindikiri, Mithika Linturi na Elizabeth Karambu.

Wengine walikuwa Alexander Mundigi (Seneta, Embu), John Paul (Igembe Kusini), Julius Taitumu (Igembe Kaskazini), John Mutunga (Tigania Magharibi), Moses Kirima (Imenti ya Kati), John Muchiri (Manyatta), Eric Muchangi (Runyenjes), Geoffrey Ruku (Mbeere Kaskazini), Nebert Muriuki (Mbeere Kusini), Jayne Kihara (Naivasha Town), Sylvanus Osoro (Mugirango Kusini), Onesmus Ngogoyo (Kajiado Kaskazini), Justus Mugo (Naibu Gavana, Embu) na MCAs zaidi ya 40 kutoka Meru na Kaunti za Embu.

Kiraitu alipoteza azma yake ya kuwania ugavana wa Meru kwa muhula wa pili katika uchaguzi wa mwezi uliopita ambapo alishindwa na mgombea huru Kawira Mwangaza.

Mwangaza alishinda kwa kura 209,148 huku Mithika Linturi wa UDA akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 183,859. Kiraitu alikuwa wa tatu kwa kura 110,814.

View Comments