In Summary

• Hakimu Wendy Muchemi alisema Mugo ni hatari kwa jamii, hivyo anafaa kuwekwa pembeni kwa muda mrefu.

Daktari James Mugo Ndichu,
Image: DOUGLAS OKIDDY

Daktari bandia Mugo wa Wairimu amehukumiwa kifungo cha miaka 29 na miezi sita jela baada ya kupatikana na hatia ya kuendesha kliniki kinyume cha sheria na kuwapa wagonjwa dawa za kulevya ili kuwadhulumu kingono.

Hakimu Wendy Muchemi alisema Mugo ni hatari kwa jamii, kwa hivyo anafaa kuwekwa mbali na jamii kwa muda mrefu.

"Yeye ni hatari kwa jamii badala ya kutumia ujuzi anaosema aliupata kuboresha jamii aliendelea kwa kujidai kuwa daktari wa wanawake na kuwapa dawa na kuwadhulumu," hakimu huyo alisema katika uamuzi wake.

Mugo alipatikana na hatia ya kuendesha kliniki kinyume cha sheria na kuwapa wagonjwa dawa za kulevya ili kuwadhulumu kingono.

Alisema Mugo aliamua kutumia vibaya ujuzi wake aliohitimu kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi kuwapa wagonjwa dawa kwa kuwapa wagonjwa wa kikie dawa za usingizi na kuwadhulumu kingono.

Katika utetezi wake, Mugo alisema alijuta kwa kuanzisha juhudi za za kutumikia jamii na nchi lakini anajuta kwa kuwa sasa yuko gerezani.

Mugo tayari anatumikia kifungo cha miaka 11 jela kwa kuendesha vituo vya matibabu visivyo na leseni.

View Comments