In Summary

•Polisi wanachunguza jinsi watahiniwa 3 waliokuwa wakifanya mtihani wa KCPE walipatikana wakiwa na simu za rununu.

•Polisi walisema afisa mmoja pia alijeruhiwa katika Shule ya Msingi ya Tawakal baada ya watu wasiojulikana kurusha mawe shuleni humo.

Maafisa wa mitihani wafungua masanduku yaliyobeba karatasi za mitihani mnamo Jumatatu, Novemba 28.
Image: ANDREW KASUKU

Mwalimu wa shule ya msingi huko Mandera Mashariki alikamatwa kwa makosa ya mtihani siku ya Jumanne.

Polisi wanachunguza jinsi watahiniwa watatu waliokuwa wakifanya mtihani wa Cheti cha Elimu ya Msingi nchini Kenya (KCPE) walipatikana wakiwa na simu za rununu.

Afisa wa uchunguzi wa jinai katika kaunti ya Mandera Benedict Kigen alisema simu hizo tatu zilichukuliwa na msimamizi katika Shule ya Msingi ya Tawakal iliyo viungani mwa mji wa Mandera.

"Tunamhoji msimimazi wa kituo ili kujua jinsi watahiniwa hawa waliingia na simu aje kwenye chumba cha mtihani," alisema.

Kigen alisema polisi wanamsaka msimamizi mwingine wa kituo anayeshukiwa kuhusika na wizi wa mtihani katika eneo la Mandera Mashariki.

Hii ilikuwa baada ya polisi kubaini kila kitu kilichotumwa kwenye simu hizo kutoka kwa shule nyingine katika eneo hilo.

Polisi walisema afisa mmoja pia alijeruhiwa katika Shule ya Msingi ya Tawakal baada ya watu wasiojulikana kurusha mawe shuleni humo.

Polisi wanashuku kuwa alishambuliwa na watu ambao walitaka kupenyeza simu za rununu lakini walikuwa wakizuiwa na umakini wao.

Watahiniwa hao watatu waliruhusiwa kuendelea na mtihani wao huku uchunguzi ukiendelea.

Hii ilikuwa baada ya kubainika kuwa chochote walichokuwa nacho, hakikuwa na athari za moja kwa moja kwenye mtihani huo, polisi na maafisa wa mitihani walisema.

Maafisa wako macho kuepusha aina yoyote ya kuvuja kwa mitihani katika zoezi linaloendelea nchini.

Timu za mashirika mengi zinafuatilia zoezi hilo.

View Comments