In Summary

•Jumla ya Sh408 milioni zimetolewa kwa Wakenya chini saa 24 tu baada ya kuzinduliwa kwa hazina ya Hustler Fund.

•Hustler Fund imeundwa mahususi kusaidia wafanyabiashara wadogo nchini.

Image: HISANI

Jumla ya Sh408 milioni zimetolewa kwa Wakenya chini saa 24 tu baada ya kuzinduliwa kwa hazina ya Hustler Fund.

Katika taarifa, Waziri wa Vyama vya Ushirika na MSMEs Simon Chelugui alifichua zaidi kuwa Wakenya milioni 1.14 kufikia sasa wamesajiliwa kwenye hazina hiyo.

Hazina hiyo imeundwa mahususi kusaidia wafanyabiashara wadogo nchini.

Rais William Ruto alizindua hazina hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu siku ya Jumatano akitimiza ahadi yake ya kabla ya uchaguzi ya kutenga Sh50 bilioni kwa ajili ya 'mahustlers.'

"Kupitia uzinduzi wa hazina hii, tunasaidia Wakenya wasio na uwezo wa kutosha kwa huduma na bidhaa zinazoitikia biashara zao na vile vile kuwakomboa kutoka kwa mawakala na kuanzisha utamaduni wa kuweka akiba, uwekezaji na usalama wa kijamii," Ruto alisema.

Hustler Fund inaundwa na bidhaa nne – za kibinafsi, biashara ndogo, SME na mikopo ya kuanzia.

Ili kupata hazina hiyo, Wakenya wanaweza kubonyeza *254# kwenye simu zao za rununu.

View Comments