In Summary

•Waliohudhuria hafla hiyo wanasikika kujibu kwa sauti kubwa kwa kupiga makofi na baadhi ya vicheko.

•Charlene amekuwa miongoni mwa mada zinazovuma na kuzua hisia kali mtandaoni Jumatano.

Binti wa kwanza wa taifa, Charlene Ruto.
Image: Facebook

Wakenya mtandaoni wanaelezea kutoamini masikio yao baada ya kusikia kuhusu kuwepo kwa afisi ya binti wa rais yenye kuhusishwa na binti wa pili wa Rais William Ruto.

Katika video inayosambazwa sana mtandaoni, Charlene Ruto anaonekana akizungumza na hadhira katika mkutano wa kilele nchini Tanzania ambapo anatambulisha “timu yake kutoka Kenya” ikiwa ni pamoja na mshauri wake na mwingine ambaye ni ” mkuu wa biashara na uwekezaji katika ofisi ya binti wa rais”.

Waliohudhuria wanaonekana kujibu kwa sauti kubwa kwa kupiga makofi na baadhi ya vicheko.

“Sielewi kinachochekesha,” Bi Ruto anajibu huku akijaribu kuendelea na utangulizi.

Sheria za Kenya hazina ofisi ya binti wa rais na hakujakuwa na tangazo lolote la umma la kuanzishwa kwa ofisi kama hiyo.

Wakenya mtandaoni wamekuwa wakikashifu kile ambacho wengine wanakiona kuwa matumizi mabaya ya pesa za walipa ushuru.

‘’Charlene Ruto akitambulisha timu yake kutoka ofisi ya binti wa rais ambaye hulipwa kwa pesa za walipa kodi licha ya kuwa ofisi isiyo halali,’’ Mkenya mmoja kwenye Twitter asema.

Mwingine anauliza jinsi ofisi hiyo ilivyoanzishwa na kushirikisha video hii:Wakenya mtandaoni wanaelezea kutoamini macho yao baada ya kusikia kuhusu kuwepo kwa afisi ya binti wa rais yenye kuhusishwa na binti wa pili wa Rais William Ruto.

Katika video inayosambazwa sana mtandaoni, Charlene Ruto anaonekana akizungumza na hadhira katika mkutano wa kilele nchini Tanzania ambapo anatambulisha “timu yake kutoka Kenya” ikiwa ni pamoja na mshauri wake na mwingine ambaye ni ” mkuu wa biashara na uwekezaji katika ofisi ya binti wa rais”.

Bi Ruto amekuwa akikutana mara kwa mara na viongozi kote nchini na kuhudhuria vikao vya kimataifa vinavyokutana na viongozi wa kigeni tangu babake awe rais.

Amekuwa miongoni mwa mada zinazovuma na kuzua hisia kali mtandaoni Jumatano.

Ameibua mijadala mtandaoni siku za nyuma huku kukiwa na mwingiliano wake wa kisiasa - na amepewa jina la utani Quickmart Ivanka kwenye Twitter, dhihaka ya kufanana kwake na Ivanka Trump, binti wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.

View Comments