In Summary

•Kelvin Kalonzo alihusika katika ajali iliyotokea katika eneo la uchunguzi la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) baada ya lori kugonga gari alilokuwamo miongoni mwa watu wengine.

•Waliojeruhiwa walikimbizwa katika hospitali huku mabaki ya gari hilo yakipelekwa kituo cha polis

Mwanawe Kalonzo Musyoka, Kevin Muasya alihusika katika ajali ya barabarani siku ya Jumamosi,, Januari 21, asubuhi.
Image: HISANI

Familia ya Kiongozi wa Chama cha Wiper, Stephen Kalonzo Musyoka imetoa shukran kwa watu ambao walichukua hatua ya kuwajulia hali baada ya mwanawe kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani siku ya Jumamosi asubuhi.

Kelvin Muasya, ambaye ni mzaliwa wa pili wa makamu rais huyo wa zamani alihusika katika ajali iliyotokea katika eneo la uchunguzi la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) baada ya lori kugonga gari alilokuwamo miongoni mwa watu wengine.

Kupitia taarifa, Mkuu wa Mawasiliano katika SKM Command Centre, BiPaloma Gatabaki amethibitisha kuwa Kelvin  na wenzake wanaendelea kupokea matibabu hospitalini baada ya kupata majeraha kutokana na ajali hiyo.

"Watu wa kwanza kufika katika eneo la tukio walikuwa wastadi na makini na tunamshukuru Mungu kwa ajili yao. Kevin na timu yake wanaendelea vizuri," Paloma alisema.

Ajali hiyo ambayo ilipelekea takriban watu wanne kujeruhiwa, akiwemo mwanawe Kalonzo inaripotiwa kutokea mwendo wa saa moja asubuhi  ya Jumamosi. Waathiriwa walikuwa wakielekea katika uwanja wa ndege wakati wa ajali, polisi walisema.

Ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa lori kushindwa kulimudu na kuligonga gari ambalo alikuwemo Kelvin  kwa nyuma.Picha zilizopigwa katika eneo la tukio zilionyesha gari hilo likiwa limeharibika vibaya.

Gavana wa Machakos, Wavinya Ndeti alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kufika katika eneo la tukio baada ya ajali kutokea. 

Waliojeruhiwa walikimbizwa katika hospitali huku mabaki ya gari hilo yakipelekwa kituo cha polisi. Uchunguzi zaidi unaendelea.

View Comments