In Summary
  • Odinga alisema hatua ya watu wengi itakuwa sehemu ya mpango wa kile alichokiita kurudisha mamlaka kwa wananchi kama ilivyoainishwa kwenye katiba
KINARA WA AZIMIO RAILA ODINGA
Image: RAILA ODINGA/TWITTER

Kiongozi wa Azimio La Umoja Raila Odinga ametaka hatua kali kuchukuliwa ndani ya siku 14 ikiwa ushuru mkubwa unaotozwa kwa bidhaa kwa sasa hautapunguzwa.

Odinga alisema hatua ya watu wengi itakuwa sehemu ya mpango wa kile alichokiita kurudisha mamlaka kwa wananchi kama ilivyoainishwa kwenye katiba.

Waziri mkuu huyo wa zamani ambaye alikuwa akizungumza katika bustani ya Jeevanje wakati wa maandamano ya maombi Jumatano alimsuta Rais William Ruto na serikali yake kwa kuandaa maombi ambayo inasema ni hatua ya kinafiki huku Wakenya wakihangaika na gharama ya juu ya maisha.

"Hawa ni wanafiki wanaomiminika kanisani kila Jumapili lakini baada ya hapo ndio watenda dhambi wakubwa," Odinga aliongeza.

"Tumezungumza kuhusu kupanda kwa gharama ya bidhaa za kimsingi kama unga, umeme, mafuta, sukari na maziwa kwa muda mrefu sana. Tumelalamikia kupanda kwa karo na kuzungumzia kuhusu watoto kuacha shule kwa kukosa karo," Raila. sema.

"Kuondolewa kwa ruzuku kwa chakula na elimu katikati ya ukame na njaa ilikuwa ya uzembe na isiyo na moyo. Kwa hivyo, ruzuku lazima zirejeshwe, na gharama ya bidhaa za kimsingi na ushuru lazima ipunguzwe katika siku 14 zijazo," Raila alisema.

Kiongozi huyo wa ODM pia alitoa wito wa kufunguliwa kwa seva ya IEBC na ukaguzi uliofanywa kwa kutumia kampuni inayotambulika.

 

 

 

 

 

View Comments