In Summary
  • Mahakama ya kazi pia imeizuia Meta na kampuni yake yaajira, Sama, kuwaajiri wasimamizi wengine wa kuchukua nafasi ya wale waliofutwa kazi.
Image: BBC

Mahakama katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, imeizuia kampuni ya Meta, ambayo ni kampuni mama ya facebook, kuwafuta kazi wasimamizi wake wa maudhui huku wakisubiri kusikilizwa kwa kesi ya kupinga hatua ya kufutwa kwao kazi.

Mahakama ya kazi pia imeizuia Meta na kampuni yake yaajira, Sama, kuwaajiri wasimamizi wengine wa kuchukua nafasi ya wale waliofutwa kazi.

Shitaka hilo liliwasilishwa na wasimamizi wa maudhui ya Facebook 43 nchini Kenya , waliokuwa wameajiriwa na Sama kwa niaba ya Meta. Wanadai kwamba shughuli ya kuwasimamisha kazi inayofanyika ni kinyume cha sheria.

Wazimamizi waliiambia mahakama kwamba wamepewamaelezo ‘’tofauti na ya ‘’kukanganya "ya kuwataka waache kazi, limeripoti gazeti la Daily Nation.

Takriban wasimamizi 260 wa maudhui walitarajiwa kufutwa kazi, kulingana na vyombo vya habari nchini Kenya.

Meta na Sama wamepewa siku saba wawe wametoa jibu kuhusu ombi hilo

Kesi hiyo itasikilizwa tarehe 28 Machi.

 

 

 

 

 

 

View Comments