In Summary

•Kiongozi huyo wa zamani wa taifa alionekana akiwa ameketi kanisani miongoni mwa waumini wengine.

•Huku kukiwa na mvutano kati ya serikali na upinzani kuhusu uvamizi huo, Uhuru ameonekana kusalia kimya.

Image: HISANI

Aliyekuwa rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alihudhuria ibada ya Pasaka mjini Mombasa siku ya Jumapili asubuhi.

Kiongozi huyo wa zamani wa taifa alionekana akiwa ameketi kanisani miongoni mwa waumini wengine.

Alishiriki katika maombi na kujiunga katika kuimba na kucheza densi.

Hii ni mara ya kwanza kwa Uhuru kuonekana hadharani tangu kuvamiwa kwa shamba la familia yake katika eneo la Ruiru.

Shamba la Northlands City lilivamiwa na watu wasiojulikana ambao waliharibu mali, kuiba kondoo na kuwasha moto mkubwa.

Viongozi mbalimbali wa kisiasa walikana kuhusika kwa njia yoyote katika uvamizi huo.

Waziri wa Usalama wa Ndani, Kithure Kindiki alisema polisi wanawasaka takriban waporaji 2,000 waliovamia shamba hilo mnamo Machi 27.

Huku kukiwa na mvutano kati ya serikali na upinzani kuhusu uvamizi huo, Uhuru ameonekana kusalia kimya.

Haya yanajiri huku viongozi wengine wakuu serikalini wakisafiri kwenda nyumbani kusherehekea Pasaka na familia zao.

Rais William Ruto na Naibu Rigathi Gachagua walisafiri hadi manyumbani mwao kuadhimisha Pasaka.

Wawili hao wanasemekana kuondoka kuelekea makazi yao ya mashambani katika kaunti za Uasin Gishu na Nyeri mtawalia siku ya Alhamisi.

View Comments