In Summary
  • Akiwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Elimu, Machogu alieleza kuwa walimu wakuu walibadilisha alama zao za chini na kuwa takwimu zisizo sahihi walizopachika kwenye mbao za matangazo.
WAZIRI WA ELIMU EZEKIEL MACHOGU
Image: ANDREW KASUKU

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu mnamo Alhamisi, Aprili 13, alifichua kwamba baadhi ya walimu wakuu katika shule mbalimbali nchini walighushi matokeo yao ya  KCPE na KCSE.

Akiwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Elimu, Machogu alieleza kuwa walimu wakuu walibadilisha alama zao za chini na kuwa takwimu zisizo sahihi walizopachika kwenye mbao za matangazo.

Aliongeza kuwa wakuu hao wa shule pia walidanganya umma kuhusu utendakazi wao akibainisha kuwa baadhi yao wakiwemo walimu wakuu wa shule za Kisii na Magharibi walizunguka na magari kusherehekea matokeo hayo ya uongo.

"Moja ya shule kama hizo ilikuwa shule ya Kitaifa huko Magharibi ambapo mwalimu mkuu alitaka kufanya ionekane kama alikuwa amefanya vyema na kuweka alama za uwongo kwenye ubao wa matangazo lakini alama zake za wastani zilikuwa chini zaidi.

"Pia kulikuwa na shule huko Kisii, na katika mojawapo, mkuu wa shule hata alizunguka na magari ya kusherehekea kwamba alikuwa na alama ya wastani ya pointi saba kitu ambacho ukweli ni kwamba alikuwa na alama ya chini," Machogu alieleza.

Waziri huyo alivilaumu vyombo vya habari kwa kusambaza habari za uongo kwamba shule katika baadhi ya maeneo haswa Kisii, Nyamira na Nyanza ndizo zilizoandikisha matokeo ya juu zaidi.

 

 

 

 

 

View Comments