In Summary
  • Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Matungulu Peter Omondi alisema kisa hicho kilitokea mwendo wa saa 3.00 asubuhi Ijumaa.
Wezi wenye sare za polisi wavamia kituo cha mafuta Machakos

Polisi wanawasaka wanaume saba ambao walinaswa kwenye CCTV wakati wa wizi ulioshindikana katika kituo cha mafuta cha Matungulu, Machakos.

Kanda ya CCTV iliyoonekana na Radiojambo inaonyesha watano kati ya wanaume waliovamia kituo cha mafuta kilichoko kando ya barabara ya Nairobi-Kangundo katika mji wa Tala.

Walikuwa wamevalia mavazi yanayofanana na ya maafisa wa polisi.

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Matungulu Peter Omondi alisema kisa hicho kilitokea mwendo wa saa 3.00 asubuhi Ijumaa.

Picha za CCTV zinaonyesha watu hao wakipora ofisi ndani ya kituo cha mafuta saa 2:09:06 asubuhi.

Omondi alisema majambazi hao walijaribu kuiba kwenye kituo cha kujaza mafuta baada ya kuwavamia na kuwafunga wafanyakazi wake wawili na kuwafungia dukani bila mafanikio.

"Hili lilikuwa jaribio la wizi katika kituo cha mafuta cha Delta ambapo majambazi saba walivamia kituo hicho cha mafuta na kuwafunga wafanyikazi na kuwafungia dukani," Omondi aliambia Star Jumamosi.

"Baadaye walianza kuvunja chumba cha usalama lakini hawakuweza kwani polisi walitaarifiwa na mhudumu wa bodaboda."

 

 

 

 

View Comments