In Summary
  • Koome, akiwa mwenyekiti wa Tume ya Huduma za Mahakama (JSC), alisema kuwa tume hiyo inachunguza rekodi hizo ili kubaini ikiwa kulikuwa na utovu wa nidhamu wa Maafisa wa Mahakama
MCHUNGAJI PAUL MACKENZIE
Image: ALPHONSE NGARI

Jaji Mkuu Martha Koome, mnamo Alhamisi, Aprili 27, alianzisha uchunguzi dhidi ya wafanyikazi wote wa Idara ya Mahakama ambao walishughulikia kesi zenye utata za kasisi, Paul Mackenzie mahakamani.

Koome, akiwa mwenyekiti wa Tume ya Huduma za Mahakama (JSC), alisema kuwa tume hiyo inachunguza rekodi hizo ili kubaini ikiwa kulikuwa na utovu wa nidhamu wa Maafisa wa Mahakama na wafanyikazi walioshughulikia suala hilo.

"Tume ya Utumishi wa Mahakama ina jukumu la kushughulikia masuala ya kinidhamu na uongozi wa Mahakama. Mahakama inasisitiza dhamira yake ya kudumisha Katiba na utawala wa sheria katika utoaji haki," alisema.

"Mahakama inatoa pole kwa familia, jamaa na marafiki wa waathiriwa walioathiriwa na vifo vingi, mateso na majeraha katika kijiji cha Shakahola kaunti ya Kilifi," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Katika taarifa kutoka kwa idara ya mahakama, kesi kadha zinazomhusu kasisi huyo mwenye utata ziliorodheshwa na jinsi alivyoachiliwa.

 

 

View Comments