In Summary

• Walinzi hao wanatoa ulinzi usiku na mchana kwa wabunge wote waliochaguliwa, maseneta, magavana na manaibu wao.

Kiongozi wa chama cha Narc Kenya Martha Karua amesema hatua ya serikali ya kuondoa walinzi wa viongozi wa Azimio ni njama ya kuwaua.

Akizungumza siku ya Jumanne mjini Nairobi, Karua alitaja kuondolewa kwa walinzi kama kinyume cha sheria.

"Jana usiku, viongozi wa Azimio akiwemo Waziri Mkuu na kiongozi wetu Raila Odinga na aliyekuwa Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka waliondolewa usalama wao," alisema.

"Huu ni ukiukaji wa upuuzaji wa katiba kinyume cha sheria, kutmia vitisho na kuhadaa. Pia wanapanga mauaji yaliyoahidiwa na Moses Kuria kwenye mtandao wake wa kijamii na kwa usemi wake hadharani" Karua aliongeza.

Alisema ofisi za Waziri Mkuu wa zamani na za Makamu wa Rais wa zamani zimehakikishiwa usalama kwa Sheria ya Bunge.

"Siyo bure. Hii ni kinyume cha sheria," Karua alitangaza.

Alisema wabunge wote wanaounga mkono mipango ya Azimio kupitia maandamano pia wamepokonywa walinzi.

Siku ya Jumanne asubuhi, maafisa wa polisi wanaowapa ulinzi Raila, Kalonzo na viongozi wengine waliochaguliwa chini ya muungano wa Azimio waliondolewa.

Kamanda wao alituma ujumbe kwa maafisa wote wa polisi wanaohusishwa na viongozi wa Azimio ikiwaamuru kuripoti kwenye idara ya polisi na kurejesha silaha zao.

“Kwa maofisa wote wa viongozi watakaoshiriki maandamano ya kesho mnashauriwa kutoandamana nao mnatakiwa kuripoti U/Camp, kurudisha silaha zenu kwenye ghala la silaha la SGB na kusalia katika Makao Makuu ya Kitengo kusubiri mawasiliano,” ujumbe huo ulieleza.

Walinzi hao wanatoa ulinzi usiku na mchana kwa wabunge wote waliochaguliwa, maseneta, magavana na manaibu wao.

View Comments