In Summary

•Ukurasa rasmi wa Kabarak University ulidukuliwa wiki iliyopita na mwanafunzi wa IT katika moja ya shule za upili nchini Indonesia.

•Chuo hicho kilifanikiwa kurejesha akaunti ya Facebook baada ya kuwa chini ya udhibiti wa mdukuzi kwa siku kadhaa.

Image: HISANI

Chuo Kikuu cha Kabarak hatimaye kilifanikiwa kurejesha ukurasa wao wa Facebook siku ya Jumanne baada ya kuwa chini ya udhibiti wa mdukuzi kutoka nchi ya Indonesia kwa siku kadhaa.

Ukurasa rasmi wa Kabarak University ulidukuliwa wiki iliyopita na mwanafunzi wa IT katika moja ya shule za upili nchini Indonesia na alikuwa anaweka machapisho yake kwa lugha ya kigeni, Kiingereza na hata Kiswahili.

Siku ya Jumanne, taasisi  hiyo ya elimu ya juu yenye makao yake kaunti ya Baringo ilithibitisha wamefanikiwa kurejesha akaunti hiyo kutoka kwa mdukuzi kwa usaidizi wa timu ya usalama wa mtandao kutoka Meta Inc.

"Mchakato wa kurejesha ulichukua usiku na siku nyingi bila usingizi, lakini timu ilidhamiria kufanikiwa na kurejesha uwepo wa chuo kikuu mtandaoni. Urejeshaji uliofanikiwa unaonyesha umuhimu wa kuwa na mfumo thabiti wa usalama wa mtandao," taarifa ya mkuu wa taasisi hiyo Henry Kiplangat ilisomeka.

Wasimamizi wa chuo hicho walitoa shukrani za dhati kwa kampuni ya Meta Inc kwa usaidizi wao katika urejeshaji wa akaunti hiyo.

"Chuo kikuu kinatazamia kuimarishwa zaidi kwa ushirikiano na Meta Inc, hasa katika mafunzo, ili kuboresha hatua zetu za usalama wa mtandao na kupanua uwezo wetu wa kuzuia na kupunguza mashambulizi ya mtandaoni," Kiplangat alisema.

Profesa Kiplangat alikiri kwamba udukuzi wa ukurasa huo ulitishia taswira na sifa ya chuo hicho kikuu mtandaoni na kusababisha hatari ya kupoteza imani kutoka kwa wadau na umma kwa ujumla.

Wiki iliyopita, mwanafunzi wa IT kutoka Indonesia alichukua udhibiti wa ukurasa uliothibitishwa wa Kabarak University wenye wafuasi zaidi ya elfu arobaini na alikuwa akipakia machapisho yake yakiwemo picha na video.

Hapo awali, alikuwa akichapisha kwa lugha ya kigeni hadi Jumamosi alipoanza kuwahutubia Wakenya kwa lugha wanayoelewa, Kiingereza, baada ya kugundua kuwa walikuwa wakifuatilia matendo yake kwa karibu.

Wiki iliyopita, mwanafunzi wa IT wa Indonesia alichukua udhibiti wa ukurasa uliothibitishwa wa Kabarak University wenye wafuasi zaidi ya elfu arobaini na amekuwa akipakia machapisho yake yakiwemo picha na video.

Hapo awali, alikuwa akichapisha kwa lugha ya kigeni hadi Jumamosi alipoanza kuwahutubia Wakenya kwa lugha wanayoelewa, Kiingereza, baada ya kugundua kuwa walikuwa wakifuatilia matendo yake kwa karibu.

View Comments