Rais William Ruto
Image: Facebook

Rais William Ruto ametetea vikali makato yake tata ya asilimia tatu kwa hazina ya nyumba akisema hii ni sawa na rehani kwa mahustler.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuweka msingi kwa mradi wa ujenzi wa makazi ya bei nafuu wa Bellevue Park mtaani South C, Nairobi, rais alipuuzilia mbali madai kwamba makato hayo yalikuwa ushuru akiyataja kama mchango na vile vile ni akiba ya matumizi ya baadaye.

Rais Ruto aliwakashifu wakosoaji wa makato yake tata akisema wakosoaji wake walikuwa wamenifaika na rehani na sasa walikuwa na nia ya kuwanyima wafanyikazi wa kipato cha chini fursa ya kuishi katika nyumba nzuri.

“Sio lazima uwe na kiwango Fulani… Tunataka hata yule mtu ambaye analipa rent ya shilingi tano aweze kulipa mortage baada ya miaka kumi na tano awe na nyumba yake,” alisema Ruto.

“Mchango mtakaotoa katika hazina ya nyumba si kodi…sio kodi, ni pesa yako, si pesa ya kodi. Ni shilingi ambazo zitakuwa maelfu, mamilioni, na mabilioni na hizo ndizo pesa tutakazotumia kujenga nyumba za bei nafuu,” aliongeza Rais.

Kiongozi huyo wa Nchi aliwashutumu wakosoaji wa pendekezo lake la ushuru wa nyumba kwa kuwapotosha Wakenya na hatimaye, kutaka kuwanyima Wakenya wa kipato cha chini nafasi ya kumiliki nyumba.

“Kila kiongozi, mbunge na MCA ana rehani. Sasa tafadhali tupange ya hao wananchi tutapanga hapo kwa housing fund. Kama wewe ni mtu unawakilisha na wewe hutaki huyo mfanyikazi awe na nafasi awe na nyumba, apatiwe na tajiri yake pesa ya kununua nyumba... wewe ni mfanyikazi ama umenunuliwa na tajiri utetee haki ya tajiri badala ya mfanyikazi?,” posed Ruto.

Mradi wa Bellevue utakuwa na jumla ya nyumba 2,356 na zitatoa ajira kwa angalau Wakenya 5000 huku rais akisema kuwa utawala wake unanuia kujenga jumla ya nyumba 200,000 kila mwaka kutoka 50,000.

Si mara ya kwanza hazina hiyo kupendekezwa. Jaribio sawia wakati wa utawala wa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta lilipingwa na Wabunge na hata wawakilishi wa miungano ya wafanyikazi.


View Comments