logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hazina ya nyumba ni 'Chama ya kitaifa' - PS Hinga

Katibu Charles Hinga ameelezea kuwa hazina ya nyumba ni kama chama cha kitaifa.

image
na

Makala15 May 2023 - 12:06

Muhtasari


• Hinga alisema Wakenya wengi watalipia shilingi 1000 kwa Hazina ambayo itafikia shilingi 84,000 kwa kila mtu katika miaka saba kwa mujibu wa Hinga.

• Katika hatua hii, Hinga alisema anaweza kuwapa Wakenya nyumba kwa riba ya asilimia 5 kwa muda wa miaka 30 kulipia mikopo.

Katibu Mkuu wa Idara ya Nyumba na Maendeleo ya Mijini Charles Hinga katika hafla ya zamani

Katibu wa kudumu wa Idara ya Nyumba na Maendeleo ya Miji Charles Hinga ameelezea kuwa hazina ya nyumba ni kama "chama cha kitaifa".

"Tuliamua kwamba ili tuweze kuafikia malengo yetu ya kuwasilisha nyumba hizo kwa bei hizo Sh5000, Sh10,000, Sh15,000, lazima tufanye jambo ambalo kila Mkenya anajua kufanya. Na hicho ni chama cha kitaifa," Hinga alisema.

Alisema kuwa mtu anayepata mapato ya juu zaidi atachangia hazina hiyo ya nyumba atalipa shilingi 2500 kila mwezi.

Hinga alisema Wakenya wengi watalipia shilingi 1000 kwa Hazina ambayo itafikia shilingi 84,000 kwa kila mtu katika miaka saba kwa mujibu wa Hinga.

"Kwa hivyo hata kunapokuwa na manung’uniko kuhusu hazina hiyo si kama tunawafilisisha Wakenya. Pesa za jumla kutoka kwa kila mtu itakua  shilingi bilioni 9 kila mwezi," alisema.

Hinga alisema serikali ikiwa na bilioni 9 kwa mwezi inaweza kuanzisha miradi nchini bila kuzingatia anachosema mwekezaji.

“Kwa sababu mwekezaji atajenga na kunikabidhi funguo na kwa kubadilishana na funguo nakupa fedha na uende,” alisema.

Katika hatua hii, Hinga alisema anaweza kuwapa Wakenya nyumba kwa riba ya asilimia 5 kwa muda wa miaka 30 kulipia mikopo.

"Mkenya ambaye yuko Maralal anaingia kwenye hiyo nyumba. Na tunaingia kwenye mkataba. Unaacha kulipa kodi ulikokuwa unalipa, ulikuwa unalipa Sh5000, nakwambia endelea kulipa hiyo hiyo kwenye mpango huu kwa miaka 30. Halafu nyumba ni yako," alisema.

Maelezo haya ya Hinga yamekuja baada ya malalamishi ya wakenya kuhusiana na hazina hiyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved