In Summary
  • Katika taarifa, Ruto alisema Eid-ul-Adha ni sherehe ya kujitolea, imani na utiifu kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.
RAIS WILLIAM RUTO
Image: TWITTER

Rais William Ruto amewatakia Waislamu siku njema na yenye furaha wanapoadhimisha Eid-ul-Adha.

Katika taarifa, Ruto alisema Eid-ul-Adha ni sherehe ya kujitolea, imani na utiifu kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.

"Siku hii yenye baraka itie msukumo wa maadili haya ya kiroho katika nyoyo za Waislamu wote na pia kuleta furaha, amani na baraka," alisema.

Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa upande wake aliwatakia Waislamu kila la kheri wanapoadhimisha siku yao maalum.

"Kwa ndugu na dada zetu Waislamu wote, nchini Kenya, na duniani kote, ninawatakia Eid-ul-Adha njema! Eid Mubarak."

Mke wa Rais Rachael Ruto aliomba siku hiyo iwaletee Waislamu furaha, amani na ustawi.

"Eid Mubarak kwa ndugu na dada zetu Waislamu wote! Natumai Eid Al-Adha hii itawaletea furaha, amani, na mafanikio. Ni roho ya kujitolea na ukarimu ambayo inafanya siku hii kuwa maalum," alisema.

Waumini wa Kiislamu walikusanyika kwa ajili ya maombi ya kuadhimisha Eid-ul-Adha.

Eid-ul-Adha ni moja ya hafla muhimu zaidi katika kalenda ya Kiislamu inayozingatiwa na mamilioni ya Waislamu ulimwenguni kote.

Sherehe ya Eid-ul-Adha inaashiria mwisho wa Hajj.

 

 

 

 

 

View Comments