In Summary
  • Siku ya Ijumaa muungano wa Azimio ulitangaza kuwa utafanya maandamano siku ya Jumatano wiki hii.
Waziri wa usalama wa ndani Kindiki Kithure wakati wa ibada ya kanisa huko Tharaka Nithi mnamo Mei 21, 2023.
Image: HISANI

Watu sita walifariki kufuatia maandamano ya Saba Saba yaliyotikisa nchi siku ya Ijumaa, Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki amesema.

Waziri huyo Jumatatu alisema maafisa kadhaa wa polisi pia walijeruhiwa wakati wa maandamano yaliyoitishwa na kiongozi wa Azimio Raila Odinga.

Alisema upinzani una haki ya kuandamana lakini si kwa gharama ya Wakenya wengine.

“Katiba inawaruhusu Wakenya kufanya maandamano lakini hairuhusu watu kubeba silaha ghafi, kuwajeruhi wengine, kutumia mawe kuziba barabara au kuchoma matairi ili kulemaza usafiri,” akasema.

Alisisitiza kwamba tabia hizo za kukithiri lazima zikome na kuthubutu upinzani kuandaa maandamano mengine siku ya Jumatano.

"Nawasubiri... Niwaambie kuwa nchi si mali yao peke yao, ni yetu sote," Kindiki alisema.

Kindiki alizungumza katika soko la Igoji alipofungua makao makuu mapya ya kaunti ndogo ya Igoji na kusimamia uwekaji wadhifa wa Naibu Kamishna wa kwanza wa Kaunti.

Siku ya Ijumaa muungano wa Azimio ulitangaza kuwa utafanya maandamano siku ya Jumatano wiki hii.

 

 

 

 

 

 

View Comments