In Summary
  • Uamuzi wa mahakama unamaanisha kuwa Sheria ya Fedha ya 2023, ambayo iliidhinishwa na Rais mnamo Juni 26 bado ni sheria isiyo na nguvu.
Omtatah apinga vikali pendekezo la kuondoa ukomo wa urais
Image: Screengrab//CitizenTV

Seneta wa Busia Okiya Omtatah sasa amedai kuwa amekuwa akipokea hadi Sh200 milioni kuondoa kesi ya Sheria ya Kupambana na Fedha ya 2023.

"Lazima tufanye ukaguzi wa madeni yetu na kulipa yale yaliyotufaidi. Yale ambayo hayajafaidi Wakenya yanapaswa kulipwa na walionufaika nayo," Seneta huyo alisema.

"Juhudi zangu za kuendelea kupigana na kusimama kwa kile ninachoamini ni sawa hazitazuiliwa."

Omtatah amesema kuwa watu wanapaswa kuhoji na kukagua madeni hayo.

"Ikiwa deni ambalo halijalipwa linachukua asilimia 70 ya bajeti yetu ya serikali, basi inataka hali ya vita," alisema.

Seneta huyo wa Busia alisema serikali iwajibike kuhusu fedha na kwamba wananchi wanapaswa kujua matumizi yake.

"Lazima tujiulize pesa hizi zinakwenda wapi," Omtatah alisema.

"Kwa hali ya ukopaji inayoendelea nchini, deni hilo litaua nchi."

Mnamo Jumatatu, utawala wa Rais William Ruto ulipata pigo kubwa ambalo linaweza kukwamisha mipango yote ya serikali baada ya Mahakama Kuu kukataa kuondoa maagizo ya kusitisha utekelezaji wa Sheria ya Fedha.

Uamuzi wa mahakama unamaanisha kuwa Sheria ya Fedha ya 2023, ambayo iliidhinishwa na Rais mnamo Juni 26 bado ni sheria isiyo na nguvu.

Mwanaharakati Okiya Omtatah na wengine wanne waliwasili mahakamani mwezi uliopita ili kupinga mswada wa fedha unaopendekezwa 2023.

Kulingana na dua lao, wanapinga kwamba mswada huo utakuwa unazidhalilisha haki ya binadamu za kiuchumi kisha kuchangia gharama kubwa katika baadhi ya bidhaa iwapo mswada huo utafanywa kuwa sheria.

“Inasubiri kusikilizwa na mahakama itakuwa radhi kutoa amri ya kusitisha mjadala kulingana na vipengele 28,30,33,36 na 76 vya mswada wa fedha mwaka wa 2023.” Akisoma karatasi za mahakama.

Pia waliisihi mahakama kutoa amri ya muda kumkataza spika wa bunge la kitaifa kukubaliana na pendekezo la rais kuukubalisha mswada wa fedha 2023 ambao unahusu vipengele vilivyotajwa.

 

View Comments