In Summary
  • Rais Ruto Alhamisi alikuwa ameonya muungano unaoongozwa na Raila Odinga dhidi ya kufanya maandamano.
MAANDAMANO Ruto atakiwa kuacha kuwaingiza mama zao kwenye mzozo wa siasa.
Image: FACEBOOK.

Rais William Ruto amesisitiza kujitolea kwake kudhibiti hali ya kutokujali, ukatili wa polisi na mauaji ya nje ya mahakama nchini.

Akiongea mjini Murang'a siku ya Ijumaa, Ruto alithibitisha kuwa jinsi alivyojitolea kuwa serikali ya Kenya Kwanza itashughulikia mauaji ya kiholela ni sawa na atahakikisha hakuna hali ya kuadhibiwa.

"Hatutaruhusu kuvunja sheria na kuuwa watu kiholela. Vile vile tulivyosema tutaondoa mauaji nje ya mahakama ni vile vile tumejizatiti kuhakikisha hakuna adhabu," alisema.

"Huwezi kuharibu mali, kusababisha ghasia na machafuko na kuepukana nayo. Huwezi. Wahalifu lazima washughulikiwe kwa uthabiti na madhubuti,"

Kauli yake ilikuja wakati maandamano dhidi ya serikali yakiingia siku ya tatu.

Rais Ruto Alhamisi alikuwa ameonya muungano unaoongozwa na Raila Odinga dhidi ya kufanya maandamano.

Akiwa Isiolo, Ruto alisema kuwa hataruhusu upinzani kuharibu Kenya kupitia maandamano.

"Sisi tunaongea kama wakenya na Sauti Moja, tumeambia wapinzani wasiharibu nchi yetu kwa kutumia," alisema.

 

 

 

 

View Comments