In Summary

• Uhuru alisema serikali inajua shughuli zake zote anazofanya Afrika nzima na kama kuna yeyote anayefikiria kuna jambo anapanga amuulize yeye sio kusumbua mamake.

Rais Uhuru akisalimiana na Mama Ngina Kenyatta katika Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo Oktoba 20, 2015
Image: HISANI

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta ameapa kufanya kila awezalo kulinda familia yake dhidi ya yeyote aliye na nia ya kuidhuru.

Uhuru ambaye ameonekana kwa umma mara ya kwanza tangu kuanza kwa maandamano yalioitishwa na muungano wa Azimio alisema hataruhusu familia yake ihangaishwe na yeyote.

Rais mstaafu alikuwa akizungumza mtaani Karen katika boma la mwanawe baada ya ripoti kudai kuwa maafisa polisi walikuwa wamevamia boma hilo kufanya msako.

Alisema yuko tayari kufanya chochote kulinda familia yake na kama kuna yeyote anayemtafuta “…kuja niko hapa wachana na familia yangu”.

Uhuru alijibu madai ya rais William Ruto kwamba alikuwa akifadhili maandamano ya Azimio, kauli ambayo pia iliungwa mkono na naibu rais Rigathi Gachagua.

Rais huyo wa awamu ya nne alisema serikali inajua shughuli zake zote anazofanya Afrika nzima na kama kuna yeyote anayefikiria kuna jambo anapanga amuulize yeye sio kusumbua mamake.

”Mimi nimestaafu, nafanya mambo yangu kwa uazi, nikiwa rais nilifanya kazi yangu niling’ang’ana kushughulikia maswala yaliyoibuliwa na wananchi kadri ya uwezo wangu, pia wewe yashughulikie mambo ya wananchi,” Uhuru alisema.

 

Uhuru alisema kwamba hajahusika kwa njia yoyote na maandamano lakini akasisitiza kwamba wakenya wana haki kikatiba kuandamana. Alisema kuwa serikali huchaguliwa kuwahudumia watu wake.

 

"Unafaa kushughulikia masuala halisi yanayowakabili Wakenya, sio kupanda juu ya magari kutoa uvumi," alisema.

View Comments