In Summary

• IG Koome alishikilia kuwa polisi wamekuwa wakifanya kile ambacho wameagizwa na katiba ambayo ni kudumisha sheria na utulivu. 

Aliyekuwa kamanda wa polisi wa Nairobi Japheth Koome
Image: MAKTABA

Idara ya polisi sasa inadai kuwa baadhi ya wanasiasa walikodisha maiti kutoka vyumba vya kuhifadhia maiti kwa lengo la kuwachafulia jina maafisa wa polisi. 

Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome amewashutumu wanasiasa hao akidai kwamba walikodisha maiti kutoka kwa vyumba vya kuhifadhia maiti na kuwaonyesha kama waathiriwa wa ukatili wa polisi. 

Siku ya Jumanne Koome alisema viongozi hao walikula njama na wahudumu wa vyumba vya kuhifadhia maiti ili kupiga picha za miili hiyo, na kisha kuziweka kwenye mitandao ya kijamii kuchafua hadhi ya idara ya polisi. 

"Taarifa nilizo nazo ni kwamba wao (wanasiasa) wanakwenda kwenye baadhi ya vyumba vya kuhifadhia maiti kuwahonga baadhi ya wafanyakazi huko," IG alisema. 

"Watu waliokufa kwa ugonjwa fulani, waliokufa labda kwa ajali au sababu zingine, wao wanapiga picha za miili kama hiyo na kuelekezea polisi lawama. Lakini hatuko katika biashara ya kujibu wanasiasa kila wakati." 

Koome alishikilia kuwa polisi wamekuwa wakifanya kile ambacho wameagizwa na katiba ambayo ni kudumisha sheria na utulivu. 

Mashirika ya kijamii na viongozi wa upinzani wameshutumiwa kwa kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa maandamano ya kupinga kupanda kwa gharama ya maisha.

View Comments