In Summary
  • Nguo zake ziliungua kabisa, na alijeruhiwa vibaya baada ya kuungua kwa angalau asilimia 50 mgongoni, mikononi na mapajani.

Mwanamume mmoja amewaacha wakazi wa kaunti ya Mombasa na watumiaji mitandao midomo wazi baada ya kujiteketeza moto huku akilalamikia ugumu wa maisha.

Kwenye video inayosambazwa mitandaoni mwanamume huyo anaonekana akiwa amebeba bendera ya Kenya kabla ya kujiwashia moto katika eneo la Mwembe Tayari, Kaunti ya Mombasa.

Manusura huyo, ambaye duru zinasema anatoka Kaunti ya Kiambu, alifika katika mzunguko wa dukakuu la Naivas na kujichoma umati uliokuwa ukipita ukishuhudia tukio hilo.

Alikuwa akilalamikia gharama ya juu ya maisha kabla ya kutekeleza kitendo hicho. Alianguka chini kutoka kwa mnara baada ya kuchomeka kwa muda.

Duru za habari zinasema kwamba mwanamume huyo alilazwa katuika hospitali ya pwani baada ya kupata majeraha kutokana na moto huo.

Wakaazi wa Mombasa walimzunguka na kusaidia kuzima moto huo.

Nguo zake ziliungua kabisa, na alijeruhiwa vibaya baada ya kuungua kwa angalau asilimia 50 mgongoni, mikononi na mapajani.

“Mimi si mwizi, sijamuibia mtu yeyote. Ninapinga kwa sababu ushindi wa Raila (katika uchaguzi uliopita wa urais) uliibiwa,” aliendelea kupiga kelele huku akihema kwa maumivu wakati watazamaji walipomhoji.

OCPD wa Mombasa Mjini Maxwell Agoro alithibitisha kwamba mwanamume huyo alikuwa ameokolewa na kukimbizwa katika Hospitali Kuu ya Mafunzo na Rufaa ya Pwani ambako amelazwa kwa matibabu.

“Tuliitwa kwenye eneo hilo na kumuokoa. Sasa tunasubiri ripoti ikamilishwe kuhusu nia gani iliyochangia uamuzi wake wa kujichoma moto,” amesema.

Agoro aliongeza kuwa hawawezi kuondoa msongo wa mawazo kwa sababu watu wengi wanatatizika.

"Hatuwezi kukataa chochote. Inaweza kuwa huzuni kwa sababu sasa hivi unaweza kufikiri mtu yuko sawa, lakini anajitahidi,” alisema.

Ripoti zingine ambazo hazijathibitishwa zinaonyesha kuwa Kioko ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Kiufundi cha Mombasa anayeendelea na kozi ya uhandisi.

Inasemekana alijaribu kujitoa uhai kutokana na hali ngumu ya kiuchumi na ukosefu wa pesa za kumuendeleza kupitia chuo kikuu

 

 

 

 

 

 

View Comments