In Summary

•Akizungumza Jumanne baada ya kuhutubia Kongamano Kuu la 36 la Baraza la Kimataifa la Kisayansi la Utafiti na Udhibiti wa Ugonjwa wa Trypanosomiasis mjini Mombasa, Naibu Rais alisema Wakenya wanastahili kutendewa kwa heshima na kusikilizwa kila wakati, hasa  katika nyakati ngumu.

Naibu Rais Rigathi Gachagua Picha: Heshima

Naibu Rais Rigathi Gachagua amewataka wafanyikazi wa umma kuheshimu Wakenya wanaposhughulikia changamoto zinazokabili nchi.

Akizungumza Jumanne baada ya kuhutubia Kongamano Kuu la 36 la Baraza la Kimataifa la Kisayansi la Utafiti na Udhibiti wa Ugonjwa wa Trypanosomiasis mjini Mombasa, Naibu Rais alisema Wakenya wanastahili kutendewa kwa heshima na kusikilizwa kila wakati, hasa  katika nyakati ngumu.

"Sote tuliopewa upendeleo wa kuhudumu tunapaswa kufanya hivyo kwa unyenyekevu. Tunapaswa kuwa na huruma na watu unaowatunza, tuheshimu walio chini yako, tuwashughulikie kwa heshima na adabu. Haikugharimu chochote," 

Aiongeza kusema kwamba  walioajiriwa katika utumishi wa umma wanapaswa kuwa makini kila mara jinsi wanavyowahutubia wananchi.

"Ikiwa unahudumia watu wa Kenya, hao ni wakubwa wako, ni waajiri wako. Unapaswa kuwaheshimu kwa jinsi unavyowahutubia," 

Naibu Rais  alisema viongozi lazima daima wabaki makini na utulivu wakati wa kushughulikia changamoto. na kuongeza kwamba sifa ya uongozi ni kutoa suluhu na kuonyesha huruma.

"Hata kunapokuwa na changamoto, muwe watulivu na thabiti na msuluhishe matatizo kwa njia ya kiutu na unyenyekevu, ili wale ambao ni wahanga wa changamoto hiyo wajisikie wanaeleweka na kuwahurumia. Hiyo ndiyo sifa ya uongozi" .

Wakati huo huo, Naibu Rais amesema Serikali iko tayari kukabiliana na changamoto zinazohusiana na mvua za Elnino zinazotarajiwa nchini mwishoni mwa mwezi huu.

Alisema ataitisha kikao na vyombo vyote vinavyohusika ili kukaza utayari wao.Akisema ataongoza kikao cha kamti ya kitaifa ya kukabiliana na dharura na washirika wa maendeleo pamoja na serikali za kaunti na wizara mbalimbali ili kubaini utayarifu wao.

 

View Comments