In Summary

•Kufuatia bei ya juu ya mafuta iliyotangazwa na serikali siku ya Alhamisi, Kuria alisema bei ya mafuta nchini itaendelea kupanda kwa angalau shilingi10 kila mwezi hadi Februari mwaka ujao,

MAANDAMANO Waziri Kuria Aomba Radhi kwa matamshi yake
Image: Twitter

Waziri wa Biashara Moses Kuria amejibu kukosolewa kwa maoni yake wiki jana kwamba Wakenya wanapaswa kutarajia bei ya juu zaidi katika  katika miezi ijayo.

Kufuatia bei ya juu ya mafuta iliyotangazwa na serikali siku ya Alhamisi, Kuria alisema bei ya mafuta nchini itaendelea kupanda kwa angalau shilingi10 kila mwezi hadi Februari mwaka ujao, na hivyo kuzua taharuki miongoni mwa Wakenya.

Miongoni mwao ni Seneta wa Kakamega Boni Khalwale, ambaye alimshutumu CS Kuria kwa kiburi.

Khalwale,alimtaka Rais William Ruto kumfuta kazi waziri huyo pamoja na Waziri wa Nishati Davis Chirchir na washauri wake wa masuala ya kiuchumi kwa ajili ya kupandisha bei ya mafuta.

Kupitia chapisho kwenye kurasa wake wa Twitter, Kuria mapema Jumatano  alisema,

"Wapendwa Wakenya, Ijumaa tarehe 15 Septemba, nilitoa maoni nikionyesha kwamba huenda bei ya mafuta ikapanda katika miezi ijayo kutokana na mabadiliko ya kimataifa. Tangu wakati huo nimeshauriwa na watu kama Dk. Boni Khalwale na bwana wake kwamba kauli hiyo haikuwa sahihi, isiyojali, na ya kiburi. Nimefanywa kuelewa sasa kwamba bei zitashuka. Naomba radhi sana kwani kukosea ni binadamu

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli wiki jana ilitangaza kwamba bei ya Super Petrol sasa imeongezeka kwa Ksh.16.96, Dizeli kwa Ksh.21.32, huku Mafuta ya Taa yakipanda juu zaidi kwa Ksh.33.13 kwa lita.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Daniel Kiptoo Bargoria alibainisha kuwa bei iliyoongezeka ilitokana na uzani wa wastani wa gharama ya bidhaa za petroli zilizosafishwa kutoka nje.

Mabadiliko yaliyofanywa Super Petrol jijini Nairobi itaanza kuuzwa kwa Ksh.211.64, Dizeli Ksh.200.99, na Mafuta ya Taa kwa Ksh.202.61 kwa lita.

View Comments