In Summary

• Waziri Kuria alisema bei ya mafuta nchini itaendelea kupanda kwa angalau Ksh.10 kila mwezi hadi Februari mwaka ujao na hata kukemea wanaolalamika  na kuwaambia wachimbe visima vyao vya mafuta.

Dr Boni Khalwale Seneta Kaunti ya Kakamega Picha: Heshima.

Seneta wa Kakamega Boni Khalwale amepuuza 'msamaha' uliotolewa na Waziri wa Biashara Moses Kuria kuhusu maoni yake kwamba Wakenya wanapaswa kutarajia bei ya juu zaidi katika miezi ijayo.

Huku kukiwa na mchepuko wa hisia tofauti kutoka kwa umma kuhusu kupandishwa kwa bei ya mafuta, Kuria alisema bei ya mafuta nchini itaendelea kupanda kwa angalau Ksh.10 kila mwezi hadi Februari mwaka ujao na hata kukemea wanaolalamika  na kuwaambia wachimbe visima vyao vya mafuta.

Hili lilivutia lawama kutoka kwa Khalwale na Naibu Rais Rigathi Gachagua ambao walimwonya Kuria na viongozi wengine kuhutubia Wakenya kwa jeuri.

Siku ya Jumatano, Kuria alirejesha maneno yake na katika chapisho lililoonekana kuwa la ulimi ndani ya shavu.  Waziri Kuria alichapisha ujumbe kwa ukurasa wake wa Twitter  akisema;

"Nimefanywa kuelewa sasa kwamba bei itashuka. Naomba msamaha sana kwani kukosea ni binadamu.Tangu wakati huo nilishauriwa na watu kama Dk. Boni Khalwale na bwana wake kwamba taarifa hiyo haikuwa sahihi, isiyojali na ya kiburi."

Akijibu matamshi ya Kuria siku ya Alhamisi kwenye kipindi cha Daybreak na Citizen , Seneta Khalwale alisema kuwa waziri huyo alikuwa mbishi na hakuwa mkweli na kuomba msamaha.

"Sijawahi jua alisoma wapi lakini nikidhani kwamba alisoma shule nzuri kama sisi wengine basi alikuwa anaandika kwa Kiingereza na kila sehemu ya ujumbe huo ni kejeli tu. Hakukuwa na msamaha hapo." 

Aliendelea kuonyesha kughadhabishwa kwake na ujumbe hu akisema kwamba atatoa uamuzi atakaposoma ujumbe wa msamaha kutoka kwake.

"Sijui alikuwa anaomba msamaha kwa nani, ikiwa ni pamoja na mimi basi hadi nisome msamaha kutoka kwake ndipo nitatoa uamuzi wa kuukubali au kuukataa."

Khalwale alikanusha zaidi maoni ya Kuria akisema kuwa ujumbe huo ulikua wa dharau, hivyo basi kuomba msamaha huo ni kama bure na kuangazia sehemu ambazo anasema zilimuudhi katika jumbe huo.

"Unaposema "watu wanapenda" ndio mwanzo wa kejeli.'Bwana wake' ni kejeli zaidi. Sisi sio wapiga ramli kujua nini kitatokea kwa bei ya mafuta akiwaambia watu waende kuchimba mafuta vizuri. aina ya kiburi hatutakaa kimya [kuhusu]," alisema.

Katika kile kilichoonekana kama shambulio lililofichwa dhidi ya Waziri Kuria, Khalwale alisema kwamba ana deni la Wakenya na wale waliomweka mamlakani tangu alipokabidhiwa wadhifa huo baada ya kukosa kunyakua kiti cha ugavana wa Kiambu katika Uchaguzi Mkuu wa 2022.

Mbunge huyo alisisitiza kuwa hatalegea kuwaita viongozi waliolala kwenye kazi zao na kuwawajibisha kwa matendo yao.

View Comments