In Summary
  • Taarifa imewasilishwa kituo cha polisi chini ya Ref OB No. 04/02/10/2023, baada ya maelezo kupokelewa na Chifu Msaidizi wa eneo hilo, Dan Kones.
Crime Scene
Image: HISANI

Msichana mwenye umri wa miaka 16 ameaga dunia baada ya kudaiwa kuvamiwa na babake katika eneo bunge la Narok Kusini, Kaunti ya Narok.

Isaiah Kibet Sawe Kipsigis, mwenye umri wa miaka 44 kutoka Jerusalem Village katika Kaunti ya Narok, anashtakiwa kwa kumpiga bintiye mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Sagamian, ambaye alikufa kutokana na majeraha alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Longisa.

Maafisa wa polisi kutoka Kituo cha Polisi cha Tendwet waliokimbilia eneo la tukio, walikutana na umati wa watu wenye ghadhabu ambao walikuwa wamemkamata mtuhumiwa na kuzuia mauaji yanayoweza kutokea.

Taarifa imewasilishwa kituo cha polisi chini ya Ref OB No. 04/02/10/2023, baada ya maelezo kupokelewa na Chifu Msaidizi wa eneo hilo, Dan Kones.

Baadaye Kibet alitiwa mbaroni na kwa sasa anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Tendwet, akisubiri kufunguliwa mashtaka rasmi.

Mwili wa marehemu ulihamishiwa katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Longisa ukisubiri uchunguzi wa maiti kubaini chanzo hasa cha kifo.

Kulingana na Citizen Digital Afisa wa Uchunguzi wa Jinai katika Kaunti Ndogo ya Narok Kusini (SCCIO) anasimamia uchunguzi unaoendelea.

 

 

 

 

View Comments