In Summary
  • Raila alisema serikali ina jukumu la kuhudumia Wakenya wote kwa usawa kwa kuwa Wakenya wote wanatozwa ushuru.

Kiongozi wa Azimio Raila Odinga amemtaka Naibu Rais Rigathi Gacgaua kuwatendea Wakenya wote kwa usawa.

Akizungumza na KTN Jumatano, Raila alisema kuwa Gachagua huwabagua Wakenya kulingana na mikoa inayodai kuwa anahudumu Mlima Kenya.

"Gachagua hastahili kuwa naibu wa rais wa Kenya kwa sababu anatoa maneno machafu ambayo inaweza kuleta kwa taifa. Yeye anasema ni naibu wa taifa la Kenya lakini yeye anajifanya naibu wa taifa la mlima Kenya," alisema.

Raila alidai kuwa DP ameangazia eneo la kati akipuuza zingine kama vile hazipo.

"Upande zile zingine za Kenya ni kigeni kwake anasema wao na sisi na anasema Kenya ni kampuni ya hisa ambapo kuna wengine wana hisa nyingi na wengine hio inaweza kugawa nchi," Raila alisema.

Aliongeza kuwa DP hafai kugawanya Wakenya kulingana na vikundi ambavyo ni vya serikali na sio.

Raila alisema serikali ina jukumu la kuhudumia Wakenya wote kwa usawa kwa kuwa Wakenya wote wanatozwa ushuru.

"Kila mtu anatozwa ushuru kwa usawa, ukitoza ushuru sukari au mafuta kila mtu analipa. Ukibagua? Hiyo ni nchi ya aina gani? Gachagua hafai kuwa DP kwa sababu ni aibu kubwa," alisema.

 

 

 

 

View Comments