In Summary

• Mahakama inafuatia ombi lililowasilishwa na mkazi wa Nandi Onesmus Kimeli,ambaye alishitaki gavana ,serikali ya Kaunti,bunge la Kaunti pamoja na AG.

• Wanane hao ambao uteuzi wao umebatilishwa ni pamoja na;Dkt Kiplimo Lagat,Philomena Kiptoo,Ruth Koech,Kibet Ronoh,Alfred Lagat,hillary Serem,Isaiah Keter na Scholastica Tuwei.

Mahakama
Image: MAHAKAMA

Mahakama ya Leba mjini Eldoret imebatilisha uteuzi wa mawaziri wanane wa Kaunti ya Nandi waliokuwa wameteuliwa na gavana Stephen Sang wa Nandi.

Gavana Sang alikuwa amewateua wanane hao Novemba mwaka jana baada ya kuchaguliwa kwa muhula wa pili.

Kesi ya kupinga uteuzi wa maafisa hao iliwasilishwa na mkaazi mmoja wa Nandi Onesmus Kimeli, ambaye alishitaki gavana,serikali ya Kaunti, bunge la Kaunti pamoja na  Mwanasheria mkuu.

Wanane hao ambao uteuzi wao umebatilishwa ni pamoja na;Dkt Kiplimo Lagat,Philomena Kiptoo,Ruth Koech,Kibet Ronoh,Alfred Lagat,hillary Serem,Isaiah Keter na Scholastica Tuwei.

Bunge la Kaunti liliidhinisha tu watu watatu kati ya wanne tarehe 14 Novemba 2022.

Kimeli aliwasilisha ombi hilo mnamo Novemba mwaka jana akiteta kuwa gavana huyo alikiuka sheria katika uteuzi huo.

Mlalamishi alidai kuwa uteuzi huo ulikiuka kanuni ya kijinsia ya thuluthi mbili na kwamba walioteuliwa pia walikosa kuafiki taaluma katika maeneo yao ya uwajibikaji.

Jaji Maurine Onyango aliamua kuunga mkono mlalamishi baada ya kusikiliza kesi hiyo.

"Ni dhahiri kutokana na yaliyotangulia kwamba gavana alilazimika kukuz usawa wa kijinsia kwa kuzingatia kanuni ya kijinsia ya theluthi mbili na hivyo kufanya uteuzi huo kinyume na matarajio ya katiba na sheria," alisema Jaji Onyango katika uamuzi wake.

Alimua kuwa watano hao wa kwanza kati ya walioteuliwa hawakuidhinishwa na bunge la Kaunti kama inavyotakiwa na sheria.

Mahakama ilibaini kuwa ikiwa gavana amechaguliwa tena ni lazima aunde kamati tendaji mpya ambayo lazima ifuate kifungu cha 35 cha sheria ya Gavana wa kaunti ilhali haikuwa hivyo Nandi.

Watendaji wanaoteuliwa tena, lazima watuliwe upya na kuhakikiwa na kuidhinishwa na bunge kulingana na namna ilivyoainishwa katika kifungu cha 42 cha Sheria.

alitoa agizo la kufutilia mbali uteui wa watendaji hao wanane kama watendaji wa kaunti na kuamuru gavana kutangaza tena nafasi hizo.

Umuzi huo wa mahakama unammanisha kuwa gavana atarejea kwenye bodi ya wahariri na kuwateua watendaji wake upya ili wakaguliwe na bunge.

 

 

View Comments