In Summary

• Magavana hao walisema kukamatwa ambako polisi walitaja kama utambulisho usio sahihi kulileta aibu kubwa, usumbufu, udhalilishaji hadharani na dhihaka kwa mwenzao.

• "Magavana ni maafisa wa serikali waliochaguliwa na wakuu wa serikali za kaunti ambao wanajulikana sana na umma. Kesi ya utambulisho usio sahihi kwa hivyo iliyowasilishwa na polisi ni ya kuchekesha."

Gavana Ann Waiguru,Mwenyekiti wa baraza la Mawaziri

Baraza la Magavana limemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome kuomba radhi kwa umma kuhusu kukamatwa kwa Gavana wa Meru Kawira Mwangaza.

"Hatua ya polisi inaonyesha mtindo wa kutatanisha wa kuwahangaisha na kuwatisha Magavana," ilisoma taarifa hiyo kwa sehemu.

"Magavana ni maafisa wa serikali waliochaguliwa na wakuu wa serikali za kaunti ambao wanajulikana sana na umma. Kisa cha kukosea katika kumtambua gavana huyo ni jambo la kuchekesha." 

Waliendelea kueleza kughadhabishwa kwao huku wakitoa ombi kwa Inspeka  Jenerali wa Polisi kumuomba gavana Mwangaza radhi hadharani.

"Tunamuomba Mkuu wa  Polisi (IG) atoe pole kwa Mwangaza hadharani kwa aibu hiyo. Tunawaomba polisi wajiepushe na kutumika kutatua masuala ya kisiasa na kutegemea ukweli na usawa katika utekelezaji wa majukumu yao."

Baraza hilo pia linamtaka IG kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya maafisa wote waliohusika katika kukamatwa kwa Mwangaza siku ya Jumatano.

Aidha Baraza hilo lilisema  litashirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ili kuhakikisha kitendo kama cha Mwangaza hairejelewi tena.

"Tungependa kutambua kwamba kuna miundo ya Serikali ya Kitaifa, kama vile maafisa wa makamanda wa kaunti ambao wanaweza kutumika kuwataka Magavana kujiwasilisha kwa polisi wakati wowote hitaji linapotokea, tunalaani vikali uonevu na vitisho na kulipiza kisasi kwamba ofisi ya Gavana lazima iheshimiwe."

Mwangaza alisema Jumatano kwamba maafisa wa polisi 'walimzuilia' ndani ya gari baada ya kudaiwa kuvuruga mpango wake wa kuzipa  masikini ng'ombe wa maziwa. 

Gavana alikuwa ametangaza kuwa alikuwa anapeana msaada wa ng'ombe kwa familia zenye uhitaji, mpango ambao polisi walidhani ulikuwa chini ya mpango wa Okolea.

"Niko chini ya ulinzi. Maafisa wa polisi hawataki kunipeleka Kituoni kufungua mastaka. Nikalishwa  kwenye gari hili la polisi kwa saa mbili sasa," alisema.

"Inasikitisha kushuhudia kupunguzwa kwa juhudi za maendeleo ambazo zimekusudiwa kusaidia walio hatarini katika jamii yetu. Vitisho kama hivyo haipaswi kuruhusiwa kutatiza maendeleo katika jamii ya Wameru," aliongeza.

View Comments