logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watanihiwa wa KCPE waliokosa kufanya mitihani wapewa nafasi ya pili kukalia mitihani hiyo

Hii itakuwa ni mara ya mwisho watahiniwa kufanya mititani ya KCPE chini ya mtaala wa 8-4-4

image
na Davis Ojiambo

Habari01 November 2023 - 09:19

Muhtasari


  • • Kwa mara ya kwanza kwa historia ya mitihani nchini,watahiniwa hao hasa wa darasa la nane watapewa nafasi ya kufanya mitihani yao baada ya zoezi hilo kukamilika .
  • • "Tutahakikisha kadiri tuwezavyo kwamba,watoto wetu wote wanaoweza kufanya mitihani watafanya mitihani,wale ambao hawataweza kufanya mitihani yao ya KCPE, tutaweza kuangalia njia ambazo kama serikali tutawasaidia watoto hawa kupiga hatua nyingine,"
Belio Kipsang,Katibu wizara ya Elimu Picha:Screengrab

Wizara ya Elimu,kupitia kwa katibu wa kudumu  Belio Kipsang,imetangaza kuwapa nafasi watahiniwa waliokosa kufanya mitihani yao mwaka huu.

Kwa mara ya kwanza kwa historia ya mitihani nchini,watahiniwa hao hasa wa darasa la nane watapewa nafasi ya kufanya mitihani yao baada ya zoezi hilo kukamilika .

Hili limezingatiwa na wizara ya Elimu hasa kwa sababu ya mitihani ya KCPE kuwa ya mwisho,wakati wakati taifa linabadilisha mkondo wa elimu na kuangazia mtaala unaozingatia umahiri CBC.

"Tutahakikisha kadiri tuwezavyo kwamba,watoto wetu wote wanaoweza kufanya mitihani watafanya mitihani,wale ambao hawataweza kufanya mitihani yao ya KCPE,tutaweza kuangalia njia ambazo kama serikali tutawasaidia watoto hawa kupiga hatua nyingine,"alisema katibu.

Alieleza kuwa ifikiapo wakati wa kutoa matokea ya mitihani ya mwaka huu,watakuwa wamepaja jawabu za taratibu za kuwasaidia watahiniwa hao.

"Kwa hivyo,kati ya sasa na wakati tutatoa matokeo ya mitihani,tutahakikisha kama serikali tumeunda taratibu za kuwasaidia watoto hawa kupiga hatua,"alieleza.

Haya yaniji baada ya visa mbali mbali vya watahiniwa kuripotiwa katika sehemu tofauti nchini.

Kaunti ya Naivasha,watahiniwa 13 ambao ni wafungwa walikosa kufanya mitihani yao.

Jumla ya watahiniwa milioni 2.6 walisajiliwa mwaka huu kukalia mitihani ya kitaifa ya KCPE na KPSEA.

Kati ya idadi hiyo,watahiniwa milioni 1.4 walisajiliwa kufanya mitihani ya KCPE huku watahiniwa milioni 1.2 wakisajiliwa kufanya mitihani ya KPSEA chini ya mfumo wa  mtaala unazingatia umahiri CBC.

Hii itakuwa ni mara ya mwisho watahiniwa kufanya mititani ya KCPE chini ya mtaala wa 8-4-4 ambao umekuwepo tangu 1985.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved