logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Babake Luis Diaz hatimaye aachiliwa huru na watekaji nyara baada ya siku 13 za wasiwasi mwingi

Kuachiliwa kwa babake Luis Diaz kunajiri siku chache tu baada ya fowadi huyo wa Liverpool kuwasihi ELN kumuacha huru.

image
na Radio Jambo

Habari10 November 2023 - 06:55

Muhtasari


•Manuel Diaz alikuwa amezuiliwa kwa siku 13 baada ya kutekwa nyara na kikundi cha waasi cha ELN mwishoni mwa mwezi uliopita.

•Kuachiliwa kwa babake Luis Diaz kunajiri siku chache tu baada ya fowadi huyo wa Liverpool kuwasihi ELN kumuacha huru.

hatimaye ameachiliwa huru.

Baba ya mshambuliaji wa Liverpool Luis Diaz hatimaye ameachiliwa huru na watekaji nyara, Shirikisho la Soka la Colombia limethibitisha.

Wanamgambo wa ELN walimkabidhi Luis Manuel Diaz kwa waumini wa kanisa katoliki na Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi mchana, na hivyo kumaliza takriban wiki mbili za wasiwasi wa kimataifa kuhusu hali yake na mahali alipo.

Alikuwa amezuiwa kwa siku 13 baada ya kutekwa nyara na kikundi cha waasi cha ELN, kwenye kituo cha mafuta cha Colombia karibu na mpaka na Venezuela mwishoni mwa mwezi uliopita.

Mama wa mchezaji huyo pia alikuwa ametekwa nyara katika tukio hilo lililotokea Oktoba 28 lakini aliokolewa ndani ya saa chache baada ya polisi kuweka vizuizi barabarani.

Ripoti za awali zilidai kuwa alitekwa nyara na mafia wa eneo hilo lakini utambulisho halisi wa waliomteka nyara ulifichuliwa tarehe Novemba 2 wakati timu ya maafisa wa serikali waliokuwa wakijadiliana na makundi ya waasi wenye silaha walisema ELN, kundi kongwe zaidi la waasi nchini humo ndilo lilikuwa limemshikilia mateka.

Kuachiliwa kwa babake Luis Diaz kunajiri siku chache tu baada ya fowadi huyo wa Liverpool kuwasihi ELN kumuacha huru.

Baada ya mchuano wa Liverpool dhidi ya Luton Town siku ya Jumapili, staa huyo wa Colombia mwenye umri wa miaka 26 alitoa taarifa kuwafahamisha watekaji nyara uchungu ambao familia yao inapitia kwa sasa.

Pia alitumia fursa hiyo kuomba kuachiliwa kwa mzazi wake huyo na kutaka mashirika ya kimataifa ya usalama kusaidia kumrejesha nyumbani.

 "Leo mwanasoka haongei nanyi, leo Lucho Díaz, mtoto wa Luis Manuel Díaz, anazungumza nanyi. Baba yangu ni mfanyakazi asiyechoka, nguzo yetu katika familia na ametekwa nyara. Kila sekunde, kila dakika, uchungu wetu unakua. Mama yangu, kaka zangu na mimi tumekata tamaa, tumefadhaika na hatuna maneno ya kuelezea kile tunachohisi,” Diaz aliandika.

Aliongeza, “Mateso haya yataisha tu tutakapokuwa naye nyumbani. Nawaomba mmuachilie mara moja, mkiheshimu uadilifu wake na mmalize kusubiri kwa uchungu haraka iwezekanavyo. Kwa jina la upendo na huruma, tunaomba mfikirie upya matendo yenu na mturuhusu kupona."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved