logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Matokeo ya mtihani wa KCPE kutolewa kabla ya Krismasi

Visa vya udanganyifu vimepungua kkwa sababu mtihani unachukuliwa mara mbili kwa siku.

image
na Radio Jambo

Habari10 November 2023 - 11:52

Muhtasari


• Katibu wa kudumu wa Elimu ya Msingi Dkt Belio Kipsang alisema usahihishaji wa KCPE umeanza huku matokeo yakitarajiwa kutoka baada ya wiki chache.

Watahiniwa wa darasa la nane wakalia mtihani wa KCPE

Wizara ya Elimu imetangaza mipango ya kutoa matokeo ya mtihani wa darasa la nane (KCPE) mapema ili kuwapa wazazi muda wa kujiandaa.

Kulingana na Wizara mtihani huo utatolewa katika muda wa wiki chache ili kuruhusu wanafunzi kuchagua shule kabla ya Krismasi.

Kulingana na katibu wa kudumu wa Elimu ya Msingi Dkt Belio Kipsang, usahihishaji wa KCPE umeanza huku matokeo yakitarajiwa kutoka baada ya wiki chache.

Akizungumza baada ya kuzuru shule ya upili ya wasichana ya Naivasha, Belio aliwapongeza walimu wakuu kwa kazi waliyofanya wakati wa mitihani ya kitaifa.

"Tunatarajia matokeo yatoke mapema ili upangaji wa wanafunzi katika kidato cha kwanza ufanyike kabla ya Krismasi na wazazi wapate muda wa kutosha wa kujiandaa," alisema.

Wakati uo huo Kipsang alipepezea chini visa vya hivi majuzi vya wizi wa mtihani wa KCSE na kuongeza kuwa ni wasimamizi saba pekee wa vituo waliosimamishwa kazi.

Alisema kumekuwa na visa vichache mno vya wizi mitihani mwaka huu kutokana mfumo wa kuchukuwa karatasi za mitihani mara mbili kwa siku pamoja na ushirikiano wa karibu na idara ya usalama.

"Tuligundua kuwa kulikuwa na ufichuzi wa vifaa vya mtihani ulipochukuliwa mara moja na kupelekea hatua ya kuichukuwa mara mbili kwa siku," alisema.

Katibu huyo wa elimu alisema kuwa wasimamizi saba wa vituo ambao walikuwa wamesimamishwa kazi na watachukuliwa hatua za kinidhamu mara tu mitihani itakapokamilika.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved