In Summary

•Waziri wa elimu Ezekiel Machogu alitangaza matokeo yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu siku ya Jumatatu asubuhi mjini Eldoret.

•Watahiniwa, wazazi na walezi sasa wanaweza kuangalia matokeo kwa kutembelea https://results.knec.ac.ke 

Waziri Ezekiel Machogu akitangaza matokeo ya KCSE 2023 mnamo Januari 8, 2023.
Image: HISANI

Ni rasmi, matokeo ya KCSE 2023 yametoka!

Waziri wa elimu Ezekiel Machogu alitangaza matokeo yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu kubwa siku ya Jumatatu asubuhi katika shule ya upili ya Moi, mjini Eldoret baada ya kukutana na Rais William Ruto katika ikulu ndogo ya  Eldoret . Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mitihani ya kitaifa kutangazwa nje ya Nairobi.

Watahiniwa, wazazi na walezi sasa wanaweza kuangalia matokeo kwa kutembelea https://results.knec.ac.ke kisha kuweka nambari ya mtihani na jina la mtahiniwa kulingana na data ya usajili wa KCSE ya 2023. 

Baada ya maelezo kuingizwa kwa usahihi, mtu anatarajiwa kuwasilisha taarifa na matokeo ya KCSE 2023 yataonyeshwa kwenye skrini.

Mfumo wa kawaida wa SMS ambao umetumika kila wakati katika miaka iliyopita hautatumika mwaka huu.

Watahiniwa wanaweza pia kupata matokeo yao kutoka kwa ofisi za elimu katika maeneo yao na shule zao baada ya kusambazwa.

Image: HISANI// KNEC

Takriban watahiniwa 903, 260 walikalia kwa mtihani wa KCSE 2023 ambao ulianza Oktoba 23, 2023 na kumalizika Novemba 2023.

Mwezi uliopita, Waziri Machogu alihakikisha kwamba matokeo yatakuwa ya kuaminika, akiongeza kuwa vituo vya kuashiria viliongezwa kutoka 35 hadi 40 ili kuboresha mazingira ya kazi.

Alisema watahiniwa hao watanufaika na mfumo mpya wa upangaji madaraja uliozinduliwa Agosti, unaolenga kuongeza idadi ya wanaojiunga na vyuo vikuu.

View Comments