In Summary

• Matokeo ya awali yanaonyesha mwanamume huyo alitumia hati bandia na nambari ya simu iliyosajiliwa kwa jina la mwanamke.

Mabaki ya mwili wa mwanamke aliyeuawa kwa kukatwa karwa katika eneo la Thika Road.
Image: SCREENGRAB

Maafisa wa upelelezi wako mbioni kumtafuta mshukiwa wa mauaji ya mwanamke mwenye umri wa miaka 24 ambaye mwili wake uliokatwakatwa ulipatikana ukiwa umeingizwa kwenye mfuko wa karatasi kando ya barabara ya Thika jijini Nairobi.

Matokeo ya awali yanaonyesha mwanamume huyo alitumia hati bandia na nambari ya simu iliyosajiliwa kwa jina la mwanamke

Kando na picha chache zilizopatikana kutoka kwa kamera za CCTV katika eneo hilo, polisi hawana la kushikilia wanapomfuatilia mshukiwa.

Sababu ya mauaji hayo bado ni kitendawili.

"Alionekana kutenda kwa hasira na tunahofia anaweza kuua zaidi," afisa katika Tkikosi cha uchunguzi alisema.

Wachunguzi wanajitahidi kutoa picha za mshukiwa zilizonaswa kwa umma ili kusaidia kumtambua.

Mwanamke huyo hajatambuliwa na polisi walichukua alama za vidole kwa uchunguzi kama sehemu ya juhudi za kumtambua.

Mwanamke huyo alidungwa kisu na kukatwakatwa hadi kufa katika nyumba iliyo karibu na TRM Drive, barabara ya Thika.

Mwanamume huyo siku ya Jumamosi alikuwa amepanga chumba na kuingia na mwanamke huyo.

Kufika Jumapili asubuhi, aliondoka peke yake, mlinzi alisema alirudisha ufunguo.

Mlinzi alienda kuchungulia nyumba na kukuta matone ya damu chumbani.

Alisema alifuata alama za damu hadi sehemu ya kukusanyia taka ambapo yeye na majirani wengine waligundua mabaki ya mtu jambo ambalo lilimfanya kupigia polisi simu.

Mwili ulikuwa umekatwa vipande vipande na kuwekwa kwenye karatasi ya plastiki.

Picha za CCTV za tukio hilo zilionyesha mwanamume aliyevalia suruali ndefu ya jeans nyeusi, fulana nyeusi, shati la samawati, madoa na kofia nyeupe akihifadhi nyumba ya chumba kimoja.

Mkuu wa polisi wa Nairobi Adamson Bungei alisema wanamsaka mshukiwa aliyehusika na mauaji hayo. Alisema mhudumu katika eneo hilo anawasaidia polisi kufanya uchunguzi.

Polisi walihamisha mabaki hayo hadi katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City mjini Nairobi wakisubiri uchunguzi wa maiti na utambulisho.

View Comments