In Summary

•Hadi kutangazwa kwa bei mpya mwezi ujao, lita moja ya petroli itauzwa kwa Ksh206.36 huku dizeli ikiuzwa kwa Ksh195.47 Nairobi.

•Hapo awali, Super Petrol iliuzwa kwa Ksh207.36, Dizeli kwa Ksh196.47, na Mafuta ya Taa kwa Ksh194.23.

Mhudumu akiweka gari Mafuta ya petroli
Image: MAKTABA

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli  nchini Kenya (EPRA) imetangaza bei mpya ya mafuta ambayo imeshukishwa kwa shilingi moja. 

Bei ya mafuta ya petroli, dizeli, mafuta ya taa sasa imeshuka hadi kwa shilingi moja kila moja kuanzia Februari 15.

Hadi kutangazwa kwa bei mpya mwezi ujao, lita moja ya petroli itauzwa kwa Ksh206.36 huku dizeli ikiuzwa kwa Ksh195.47 jijini Nairobi. Mafuta ya taa, kwa upande mwingine, yatauzwa kwa Ksh 93.23 kuanzia Februari 15.

Hapo awali, Super Petrol iliuzwa kwa Ksh207.36, Dizeli kwa Ksh196.47, na Mafuta ya Taa kwa Ksh194.23.

Wakati ikitangaza bei mpya, EPRA ilibaini kuwa bei hizo mpya ni pamoja na asilimia 16 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kama ilivyoainishwa na Sheria ya Fedha ya 2023, Sheria ya Kodi (Marekebisho) ya Sheria ya 2020.

Haya yanajiri huku shilingi ikionekana kuendelea kuimarika dhidi ya dola baada ya kudorora kwa zaidi ya mwaka mmoja .

Kulingana na Benki Kuu ya Kenya, kiwango cha ubadilishaji cha Dola ya Marekani dhidi ya Shilingi ya Kenya  ilikuwa ni Ksh158.66 mnamo siku ya Jumatano.

Kwa kipindi cha zaidi ya wiki moja mfululizo, Benki kuu ya Kenya (CBK) ilifichua kuwa shilingi imeendelea kuimarika, ikihusisha faida hiyo kutokana na fedha za kigeni na sekta ya Utalii inayostawi.

View Comments