In Summary
  • Katika taarifa yake , Ruto alielezea rambirambi zake na mshikamano wake na watu wa Iran katika wakati huu mgumu.
Rais wa Iran Ebrahim Raisi
Image: BBC

Rais William Ruto amemuomboleza mwenzake wa Iran Ebrahim Raisi aliyefariki katika ajali ya helikopta Jumapili, Mei 19.

Katika taarifa yake , Ruto alielezea rambirambi zake na mshikamano wake na watu wa Iran katika wakati huu mgumu.

Ruto alimkumbuka Rais Raisi kama kiongozi asiye na woga na mtumishi wa umma aliyejitolea na kazi iliyotukuka katika utumishi wa umma.

"Ningependa kutoa rambirambi zangu za dhati na mshikamano na watu wa Iran katika wakati huu mgumu," Ruto alibainisha.

Alimtaja kama kiongozi madhubuti aliyejitolea kwa mambo ambayo aliamini na alijaribu kuinua hadhi ya Iran katika jukwaa la kimataifa.

Ruto zaidi alibainisha kuwa Kenya na Jamhuri ya Iran zina uhusiano wa kindugu na ziara ya Raisi nchini Kenya Julai 2023 ikiwa ni safari ya kwanza kabisa barani Afrika kama Rais.

"Tunapowapa pole watu wa Iran, tunapongeza rehema za Mwenyezi Mungu na faraja kwa watu wa Iran," Ruto alisema.

Raisi alikuwa kwenye helikopta iliyoanguka katika eneo la milima kaskazini-magharibi mwa Iran siku ya Jumapili.

 

 

 

 

View Comments