In Summary

"Kwa sababu leo, tulipokuwa tukizunguka, aliniambia unaona nilichokuambia? Na ni tofauti kabisa," Ruto alisema.

Mkewe Rais Rachel Ruto, Rais William Ruto walipokutana na Mtangazaji wa Televisheni ya Marekani Steve Harvey katika Studio za Tyler Perry mnamo Mei 21, 2024. Picha: NANCY AGUTU

Rais William Ruto siku ya Jumanne alimuomba msamaha bintiye kwa kukataa kumruhusu kusomea filamu.

Katika ufichuzi alioutoa baada ya kutembelea studio za Tyler Perry, Ruto alisema mmoja wa binti zake alitoa ombi hilo takriban miaka minane iliyopita, na hakuelewa lolote kuhusu kozi hiyo.

Aliongeza kuwa walipokuwa wakizuru studio za Tyler Perry, binti huyo alimkumbusha.

Baada ya ziara hiyo, Rais alisema sasa ana mawazo tofauti kuhusu filamu.

“Sasa nimeelewa miaka 8 iliyopita, binti yangu na yupo karibu aliniuliza ‘unajua nataka kufanya filamu’ nikamuangalia ulisemaje, lazima nimuombe msamaha leo, alikuwa sahihi na nilikosea.

"Kwa sababu leo, tulipokuwa tukizunguka, aliniambia unaona nilichokuambia? Na ni tofauti kabisa," Ruto alisema.

Rais Ruto ambaye yuko katika ziara ya siku nne nchini Marekani ikiwa ni pamoja na ziara ya kiserikali alikutana na wadau wa tasnia ya filamu ili kutafuta njia za kushirikiana na kukuza tasnia ya filamu nchini.

Katika studio za Tyler Perry, Ruto na ujumbe wake walipokelewa na mtangazaji wa TV wa Marekani, Steve Harvey.

Tangu alipowasili Marekani Jumatatu, Rais Ruto amefanya mikutano na zaidi ya mashirika 10 na makundi tofauti, wakiwemo Wakenya wanaoishi Amerika.

IMETAFSIRIWA NA DAVIS OJIAMBO. 

View Comments