In Summary

• Mwanaharakati Boniface Mwangi aliwasihi Wakenya kuendeleza vita dhidi ya uongozi mbaya.

• Serikali inashikilia kuwa ni  watu 25 pekee waliuawa katika maandamano kote nchini, na kupinga takwimu za Mashirika ya Haki za binadamu.

• Mashirika ya Haki za binadamu yalisema kuwa zaidi ya watu 40 walifariki.

Image: HISANI

David Chege, mmoja wa vijana waliouawa wakati wa maandamano ya kupinga msuada wa fedha nchini, alizikwa siku ya Jumanne nyumbani kwao eneo la Gatundu.

Chege ambaye alipigwa risasi kichwani alikuwa mtaalamu wa IT na mwalimu wa Sunday School katika Kanisa la Jubilee Christian Church.

Chege alikuwa miongoni mwa wakenya waliouawa kwa kupigwa risasi nje ya majengo ya bunge wakati waandamanaji walipozidi polisi nguvu na kuingia katika majengo ya bunge.

Mazishi yake yalihudhuriwa na wanaharakati wengi miongoni mwao  Boniface Mwangi, Hanifa Adan  na Khalid Hussein wa Haki Afrika.

Image: HISANI

Wakati wa mazishi wanaharakati waliikabidhi familia yake bendera, wakisema kuwa marehemu Chege alilipa gharama kubwa kwa uzalendo wake.

Mwanaharakati Boniface Mwangi aliwasihi Wakenya kuendeleza vita dhidi ya uongozi mbaya, akiwataka wabadilishe picha ya Rais Ruto na picha ya bendera ya Kenya.

Serikali inashikilia kuwa ni  watu 25 pekee waliuawa katika maandamano kote nchini, na kupinga takwimu za Mashirika ya Haki za binadamu ambayo yalisema kuwa zaidi ya watu 40 walifariki.

View Comments