In Summary
  • Ripoti ya polisi siku ya Jumamosi ilisema kuwa nyoka huyo aliuawa na kuchomwa moto na babu wa mtoto huyo Salim Mwendwa ndani ya boma lao.

Mtoto wa miaka 3 amefariki baada ya kudaiwa kula mabaki ya nyoka aina ya green mamba katika kijiji cha Kavuvwani B, lokesheni ya Kavuvwani, Kaunti ya Kitui.

Ripoti ya polisi siku ya Jumamosi ilisema kuwa nyoka huyo aliuawa na kuchomwa moto na babu wa mtoto huyo Salim Mwendwa ndani ya boma lao.

Inasemekana mtoto huyo alikula mabaki ya nyoka huyo akiwa chini ya uangalizi wa nyanya Margret Nzangi Mwendwa.

Salim alikimbia kuripoti kisa hicho katika kituo cha Polisi cha Mwingi jambo ambalo liliwafanya maafisa kutembelea boma hilo na kuandika kumbukumbu za tukio hilo.

Mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Mwingi Level IV ukisubiri uchunguzi wa maiti.

 

 

 

 

View Comments