In Summary

•Kuria alifichua yeye na Kiunjuri walikutana katika hoteli moja isiyofichuliwa ambapo mbunge huyo alimnunulia chakula cha mchana.

•Kuria alimshukuru mbunge huyo kwa kitendo hicho na kubainisha kuwa walikuwa na mkutano mzuri wa chakula cha mchana.

Image: TWITTER// MOSES KURIA

Aliyekuwa waziri wa utumishi wa umma, usimamizi wa utendakazi na utoaji huduma, Moses Kuria na Mbunge wa Laikipia Mashariki Festus Mwangi Kiunjuri walifanya mkutano Jumatano.

Kuria alitumia akaunti zake za mitandao ya kijamii kufichua kuwa yeye na Kiunjuri walikutana katika hoteli moja isiyofichuliwa ambapo mbunge huyo alimnunulia chakula cha mchana.

Alidokeza kuwa Kiunjuri alifanya kitendo hicho kama ishara ya kumfariji kufuatia kutimuliwa kwake katika baraza la mawaziri, kitendo ambacho waziri huyo wa zamani pia alimfanyia alipotimuliwa kutoka kwa baraza la mawaziri la aliyekuwa rais, Uhuru Kenyatta mnamo Januari 2020.

"Tarehe 14 Januari 2020 rafiki yangu Festus Mwangi Kiunjuri alifukuzwa kwenye Baraza la Mawaziri. Siku hiyo nilimpeleka kwa chakula cha mchana. Leo kaka yangu amerudisha neema hiyo,” Kuria aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter.

Kuria alimshukuru mbunge huyo kwa kitendo hicho na kubainisha kuwa walikuwa na mkutano mzuri wa chakula cha mchana.

Mnamo Julai 11, Rais William Ruto alivunja baraza lake la mawaziri akiwemo Moses Kuria ambaye alikuwa akihudumu kama waziri wa utumishi wa umma, utendakazi na usimamizi wa utoaji huduma.

Ruto kufikia sasa amewateua watu ishirini kuchukua nyadhifa tofauti katika baraza la mawaziri lakini Moses Kuria bado hajarejeshwa.

Jumatano asubuhi, Rais William Ruto Jumatano alitangaza hadharani orodha yake ya pili ya walioteuliwa kuchukua nyadhifa kwenye Baraza la Mawaziri.

Uteuzi huo unajiri wiki kadhaa baada ya Rais kulivunja baraza lake lote la mawaziri isipokuwa Waziri Mkuu Musalia Mudavadi.

Orodha ya mwisho inajumuisha;

  • Wizara ya Fedha - John Mbadi
  • Wizara ya Vijana na  Michezo - Kipchumba Murkomen
  • Wizara ya Vyama vya Ushirika - Wycliffe Oparanya
  • Wizara ya Jinsia, Utamaduni na Urithi - Stellah Langa't
  • Wizara ya Utalii - Rebecca Miano
  • Wizara ya Nishati - Opiyo Wandayi
  • Wizara ya Utumishi wa Umma - Justin Muturi
  • Wizara ya Biashara - Salim Mvurya
  • Wizara ya Kazi - Alfred Mutua
  • Wizara ya Madini - Hassan Joho

Siku ya Ijumaa wiki jana, rais alitaja kundi la kwanza la walioteuliwa kwenye baraza lake la mawaziri akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

  • Wizara ya Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa - Kithure Kindiki
  • Wizara ya Afya - Debra Mulongo Barasa
  • Wizara ya Ulinzi- Aden Duale
  • Wizara ya Barabara na Uchukuzi - Davis Chirchir
  • Wizara ya Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu - Soipan Tuya
  • Wizara ya Maji, Usafi wa Mazingira na Umwagiliaji - Eric Muga
  • Wizara ya Elimu- Julius Migosi
  • Wizara ya Ardhi, Kazi za Umma, Nyumba na Maendeleo ya Miji - Alice Wahome
  • Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo- Dk Andrew Karanja
  • Wizara ya Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali- Dk Margaret Ndungu

Rais Ruto alimteua Rebecca Miano kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Miano hata hivyo amehamishwa kupelekwa wizara ya Utalii.

View Comments