In Summary

•Ndege zilizopaswa kutua JKIA zitalazimika kutua hadi Mombasa na Kilimanjaro kutokana na ukungu uliosababisha kutoonekana vizuri

•Safari tisa za ndege zilielekezwa kutoka JKIA, nne zilighairiwa na nne kucheleweshwa kkutokana na hali mbaya ya hewa.

Ndege ya Kenya Airways
Image: HISANI// KENYA AIRWAYS

Ndege zilizokuwa zimepangiwa kutua katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA)  mapema siku ya Alhamisi zililazimika kutua uwanja wa kimataifa wa Mombasa au Tanzania kutokakana na ukungu mkali jijini Nairobi. 

Shirika la ndege la Kenya Airways katika taarifa yake siku ya Alhamisi asubuhi liliekeza  ndege zake zilizokuwa zimepangiwa kutua JKIA katika viwanja mbadala.

Katika taarifa, KQ ilieleza kuwa abiria wanapaswa kutarajia kucheleweshwa kwa kuondoka na kuwasili Nairobi lakini iliwahakikishia kuwa hatua zote zinachukuliwa kwa ajili ya ustawi wao na pia usalama wao ambao ni muhimu.

"Tunapenda kuwafahamisha wateja wetu kwamba asubuhi ya leo, tumeelekezwa hadi Mombasa na Kilimanjaro.

Baadhi ya safari zetu za ndege zilikuwa zimepangwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Hii ni kutokana na kutoonekana vizuri kulikosababishwa na hali mbaya ya hewa," ilisema taarifa hiyo kwa sehemu.

"Kutokana na hilo, tunatarajia ucheleweshaji wa kuondoka na kuwasili katika jiji kuu la Nairobi.

Tunaelewa kuwa hali hii inaweza kusababisha usumbufu na kero, ila tumehakikisha  kuwa tumechukua hatua zote muhimu za usalama na ustawi wa wafanyakazi wetu, na wateja ndio nambari yetuna kipaumbele cha kwanza."

Ukaguzi wa moja kwa moja kwenye Flight Radar 24 ulionyesha kuwa kuanzia saa 5:00 asubuhi, safari tisa za ndege zilielekezwa kutoka JKIA, nne zilighairiwa na nne kucheleweshwa kutokana na hali mbaya ya hewa.

View Comments