In Summary

Vipaumbele vya Raila katika usukani wa AU vitajumuisha:

• Ushirikiano wa Afrika na Maendeleo ya Miundombinu,

• Mabadiliko ya Kiuchumi,

• Kuimarisha Biashara ya Ndani ya Afrika  na 

• Uhuru wa Kifedha.

KINARA WA UPINZANI RAILA ODINGA
Image: EZEKIEL AMING'A

Serikali ya Kenya imewasilisha rasmi nyaraka za kumuunga mkono mgombea wake, Raila Odinga, katika azma yake ya kuwa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC).

Wakiongozwa na Katibu Mkuu wa wizara ya mashauri ya kigeni Korir Sing'oei, wajumbe wa Kenya waliwasilisha hati hizo kwa Mkuu wa Kanda ya Mashariki, Dharmraj Busgeeth na kwa Ofisi ya Wakili wa Kisheria wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa.

Kulingana na Sing'oei, vipaumbele vya Raila katika usukani wa AU vitajumuisha; Ushirikiano wa Afrika na Maendeleo ya Miundombinu, Mabadiliko ya Kiuchumi, Kuimarisha Biashara ya Ndani ya Afrika, Uhuru wa Kifedha, Usawa wa Jinsia na Usawa, Mageuzi katika kilimo Hatua za Hali ya Hewa, Amani na Usalama na Ajenda ya kuwazesha vijana Afrika.

View Comments