logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kasisi wa kanisa la 'kufunga hadi kufa' Paul Mckenzie akana mashtaka ya mauaji

Kasisi huyo na wenzake wanakabiliwa na mashtaka mengi ya kuua bila kukusudia katika mauaji ambayo yamepatiwa jina la mauaji ya Shakahola.

image
na Samuel Maina

Habari12 August 2024 - 12:47

Muhtasari


  • •Kasisi huyo na wenzake wanakabiliwa na mashtaka mengi ya kuua bila kukusudia katika mauaji ambayo yamepatiwa jina la mauaji ya Shakahola.
  • •Takriban mashahidi 420 wameandaliwa na upande wa mashtaka huku kesi hiyo ikipangwa kuendelea kwa siku nne hadi Alhamisi.
Mchungaji Paul Mackenzie

Kiongozi wa kanisa la kufunga hadi kufa nchini Kenya Paul McKenzie amekana mashtaka ya Mauaji ya kutokusudia kufuatia vifo vya waumini zaidi ya 400 katika mkasa unaohusiana na ibada katika pwani ya Kenya.

McKenzie pamoja na washukiwa wengine 94, walifikishwa mahakamani mjini Mombasa leo siku ya Jumatatu na kukanusha mashtaka.

Kasisi huyo na washtakiwa wenzake wanakabiliwa na mashtaka mengi ya kuua bila kukusudia katika mauaji ambayo yamepatiwa jina la mauaji ya Shakahola.

McKenzie ambaye alikamatwa Aprili iliyopita, baada ya miili kugunduliwa katika Msitu wa Shakahola, anatuhumiwa kuwahimiza wafuasi wake wafe kwa njaa ili "kumlaki Yesu," habari iliozua mshtuko mkubwa nchini Kenya na kote duniani.

Mwendesha mashtaka Alexander Jami Yamina amesema kuwa kesi hiyo ni ya kipekee nchini Kenya, na washukiwa watashtakiwa chini ya sheria inayohusiana na makubaliano ya kujitoa uhai.

Takriban mashahidi 420 wameandaliwa na upande wa mashtaka huku kesi hiyo ikipangwa kuendelea kwa siku nne hadi Alhamisi.

Mwezi Machi mwaka huu, mamlaka ilianza kutoa miili ya baadhi ya waathiriwa kwa ndugu zao baada ya miezi kadhaa ya kazi kubwa ya kuwatambua kwa kutumia chembechembe za DNA. Hadi sasa milii 34 imerejeshwa.

Mackenzie alikuwa ameanzisha Kanisa lake la Good News International Church mwaka wa 2003, lakini akasema alilifunga mwaka wa 2019 na kuhamia Shakahola kujiandaa na kile alichotabiri kuwa mwisho wa dunia Agosti mwaka jana.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved