In Summary

• Wafanyabaishara hao wamechoma magurudumu ya gari katika sehemu kadhaa za barabara wakisambaratisha uchukuzi wa kuingia na kutoka katikati mwa jiji la Nairobi.

• Barabara za Jogoo na Haile Sellasie ndizo zimeathirika mno.

Picha Polisi warusha vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji jijini Nairobi, Alhamisi 12, 2024
Image: Brian Oruta

Shughuli za kawaida zimesambaratika asubuhi ya Alhamisi baada ya kundi la wafanyabiashara katika soko la Marikiti kukabiliana na polisi.

Makabiliano haya yalitukia baada ya wafanyabiashara hao kufunga baadhi ya sehemu za barabara  hiyo kuingia katikati mwa jiji la Niarobi kuelezesa kutofurahishwa kwao na mpango wa kuwahamisha hadi soko la Kangundo.

Wafanyabiashara hao walichoma magurudumu barabarani kuzuia uchukuzi wa kuingia  na kutoka katikati mwa jiji la Nairobi.

Barabara zilizoathirika zaidi ni Jogoo na ile ya Haile Sellasie.

Kufikia wakati taarifa hii inachipishwa hakuna gari kutoka upande wa Jogoo Road linaweza kuingia katikati mwa jiji. 

View Comments