In Summary

• Washukiwa wa wizi wa kimabvu wakamatwa mchana wa Ijumaa katika eneo la moja kaunti ndogo ya Rongai.

• Walikamatwa na simu nne pamoja na vifaa vinavyodaiw kutumika kutelekeza uhalifu ikiwemo mitaimbo na koleo.

police car
Image: hisani

Washukiwa wawili wa wizi wa kimabavu wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Menengai katika kaunti ya Nakuru.

Wawili hao kwa jina Collins Masira Michira na Cornelius Audi Odhiambo walikamatwa na maafisa wa DCI katika eneo la Mercy Njeri kaunti ndogo ya Rongai mnamo Ijumaa mchana.

Taarifa ya polisi inadai kuwa wawili hao wanahusishwa na msururu wa wizi wa kimabavu katika eneo la Ngata na polisi walifanikiwa kuwakamata baada ya upepelezi wa maafisa wa DCI kufanywa.

Polisi walifanikiwa kupata bidhaa zinazodaiwa kuwa za wizi latika gari walilokamatwa nalo.

Simu nne, viatu na nguo za watu wakubwa na watoto zinazoaminika kuwa za watu walioibiwa zilipatikana katika gari lao.

Vile vile, vifaa vya kutekeleza wizi ikiwemo kisu, panga, mtaimbo na koleo za kazi nzito zilipatkana kwenye gari.

Vifaa hivyo vinadaiwa kutumika kuvunja nyumba wanazoiba na kusababisha majeraha kwa waathiriwa wanaokumbana nao.

Idara ya DCI imewashukuru wananchi kwa kushirikiana nao kumaliza visa vya uhalifu.

Washukiwa wanazuliwa kwenye seli za polisi wakisubiria kufikishwa mahakami kujibu madai dhidi yao.

 

View Comments